BREAKING NEWS:NDEGE YA ETHIOPIA YATEKWA NYARA LEO



Ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa hadi Rome Italia ,imetekwa nyara na kulazimishwa kubadili mkondo wake na kutua mjini Geneva Uswisi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote wako salama . 

Ndege hiyo imetua Geneva kulingana na msemaji wa Shirika la ndege la Ethiopia katika uwanja huo wa ndege. 

Haijulikana hadi sasa ni nani aliyeiteka nyara ndege hiyo wala anataka nini. 
Maafisa wa uwanja huo wa ndege wanasema kuwa wamemtia mbarani mmoja kati wateka nyara hao.
Uwanja wa ndege wa Geneva umefungua kwa sasa. Ndege hiyo yenye usajili wa Flight 702 iliondoka Addis Ababa saa sita u nusu na ilikuwa inatarajia mjini Rome saa kumi na moja kasro dakika 20 alfajiri .
One hijacker has been arrested, according to an airport spokesman quoted by Swiss newspaper Tribune de Geneve on its website.
Tutakujuza habari zaidi pindi tutakapo aarifiwa .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: