UONGO HUSAIDIA WAKATI MWINGINE: SOMA HAPA ZAIDI UTANIELEWA
UONGO UNAOKUBALIKA
Upo uongo unaokubalika rafiki zangu. Unajua kuna baadhi ya mambo ukiyasema kwa usahihi kama yalivyo yanaweza kuleta athari kwenye uhusiano, ndiyo maana nimesema kwamba upo uongo unaokubalika.
Inawezekana umefanya kitu ambacho hakimpendezi mpenzi wako, ama kwa kujua au kutokujua, lakini baada ya kuhisi labda amegundua na kukuuliza, unakataa. Ukikubali kwa kitu ambacho hakipendi inaweza kusababisha penzi kuvunjika.
Unabaki kuwa uongo mtamu kwa sababu kwanza una lengo la kulinda penzi, lakini pia hauna madhara kwa mpenzi wako. Huo ndiyo uongo mtamu ninaouzungumzia hapa.
Kutokana na nafasi yangu kuwa finyu, kwa leo naomba kuishia hapa. -GPL
0 comments: