MUME WA AUNT EZEKIEL ATIWA NDANI HUKO DUBAI


Habari ambazo zimetufikia hivi punde ni kwamba yule shemeji wa wana Bongo Movie na walimbwende hapa nchini Papaa Sunday Demonte ambaye alimuoa Aunt Ezekiel yupo sero hivi sasa katika moja ya viunga vya dola vya Dubai. Taarifa hii kutoka chanzo chetu cha uhakika cha karibu na Pendeshee huyu wa magari kutoka huko Dubai zinasema Pendeshee huyu amekamatwa kwa madai mbalimbali likiwemo la kuto kuishi kihalali katika Nchi hiyo kwa kipindi kirefu ambayo ni maarufu kwa biashara duniani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu Papaa huyu alikuwa akisakwa muda mrefu sana, ata wakati anafunga ndoa na Aunt Ezekiel alikuwa akiishi kimashaka mashaka kwa kuogopa kuingia katika mikono ya dola ya waarabu hao. Mtandao huu umejitahidi kumtafuta Aunt Ezekiel ili kumuuliza kama taarifa hizi anazo, ila simu yake haikupatikana mpaka tunaingia mitamboni, vile vile mtandao wako unajaribu kuwasiliana na mwakilishi wetu wa serikali nchini humo Bwana Omary Mjenga ili kuweza kujua kama wana taarifa yoyote ya kukamatwa kwa mtanzania huyu na nini wanatakiwa kufanya ili kuweza kujua chanzo kikuu na nini hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa za kuweza kumsaidia.

Taarifa zaidi tutawajulisha pindi tutakapowapata watu wengine ambao tunawatafuta ili kuweza kujua ni nini cha kufanya ili kumuwezesha atoke na kuweza kuishi salama salmin.

Source:Niaje Tanzania
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: