MUME WA JACK (JACQUELINE PENTEZEL) AMMWAGIA SIFA MKEWE...!!

MUME wa mwigizaji, Jacqueline Pentezel, Gardner Dibibi, amemmwagia sifa kibao mkewe akidai tangu afunge ndoa miezi nane iliyopita, hajawahi kuonja chakula cha mtaani kama ilivyokuwa zamani. 
 Akizungumza na paparazi wetu nyumbani kwake Mwananyamala, jijini Dar, Garder alisema watu walikuwa wakimchukulia tofauti sana mkewe lakini kiukweli ni mke bora na ni mtaalamu kupika.

“Mke wangu ni zaidi ya mke, ni tofauti na watu wanavyomchukulia na ni mtaalamu wa jikoni. Sijutii hata chembe kumuoa,” alisema Gardner
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: