KWANINI PENZI LA MBALI LINANOGA KULIKO PENZI LA KARIBU


Wadau nimeona niwashirikishe hili jambo ili wale wataalam wa malavidav watupe utaalamu wao
kwanini Penzi la Mbali huwa linanöga kuliko penzi la karibu nikiwa na maana kwamba; 

kama una mpenzi wako mnaishi umbali wa kuweza kusitisha shughuli zako japo kwa siku mfano arusha-dar ili muonane, hisia zake ni kubwa na kuheshimiana kunakuwepo sana kuliko yule wa pale mtaani?

Wanandoa ambao hawakai pamoja wengi wao wanaheshimiana zaidi kuliko wale wanaoishi pamoja?

Mkianzisha mahusiano katika hali yoyote kabla ya kuonana au kufahamiana mnaonyeshana lv sana, ila mkikutana tu hata kama ni sms mlikuwa mnatumiana zinapungua?

Ni Theory gani inafaa kutumika hapa?
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: