Awashangaa wanaotaka Zanzibar iendelee kuwa manispaa, asema kutokuwepo Serikali ya Tanganyika ndio kero Kuu ya Muungano ,awasuta wanaotaka Serikali Mbili
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar leo amesema
lengo la kuandikwa kwa Katiba Mpya si kuyafanyia Marekebisho katiba
iliyokuwepo sasa bali ni kuandika Katiba Mpya katiba ambayo itakuwa
Muarubaini kwa kero za Muungano na Muungano wenyewe.
Mwanasheria Mkuu aliyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akifungua
Baraza la Katiba la Vyuo Vikuu liliondaliwa na ZAHILFE Shirikisho la
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar liliofanyika katika Ukumbi wa Salama
Hal Bwawani.
Alilisifu Baraza hilo na kusema kuwa ni Baraza la Vijana wasome na
kuwasifu Vijana kwa ile sifa yao kubwa ya kuleta mapinduzi katika jamii
yeyote.
Alimtaja kijana Sir King ndie waliosababisha Zanzibar iiteme
Tanganyika mwaka 1895 Ogast na Tanganyika kuangukia katika mikono wa
Wajerumani.
Na kumtaja Gerald Pota alietumwa na Waingereza kuja kuunda Serikali
na kumpangia Mfalme mshahara ambako alikuwa akilipwa paund 250 kwa
mwaka.
Msingi wa Muungano wa Tanzania ni kuungana kwa Nchi mbili huru
Tanganyika na Zanzibar lengo la kuungana kwa nchi mbili hizi ni kufanya
mambo yao pamoja na kupata faida zaidi na sio Nchi moja kuitawala Nchi
nyengine alisema, hukua akiendela kusema:
Zanzibar si mkowa wala wilaya, Zanzibar ni Nchi, katika Muungano
tulikubaliana baadhi ya mambo kufanya pamoja na sio Zanzibar kuwa Jimbo
la Tnganyika.
Alisema duniani kuna miungano mingi mizuri akiutolea mfano Muungano
wa Uswis ambao una Serikali 24 na ule wa Muungano wa Maerkali wenye
Serikali 52 na kusema kuwa ni uongo kuwa Serikali Tatu zitavunja
Muungano na kusema Serikali Mbili ndizo zitakazovunja Muungano, na hata
Muungano wa Serikali Tatu ukivunjika si kioja.
Serikali Tatu hazitovunja Muungano Serikali Mbili ndizo zitakazo vunja Muungano.
Alisema Uruhani wa Serikali ya Tanganyika ndio kero kubwa ya Muungano
na Serikali tatu itairudisha Serikali ya Tanganyika ambako kero kubwa
itakuwa ishatatuliwa.
Aliitaja Sheria ya Kuanzishwa na Bank Kuu ya Tanzania kuwa aliisaini
Karume mwenyewe lakini Karume alipoona mapungufu ya Seria hiyo ndio
maana akaanzisha PBZ.
Aidha alisema kama Zanzibar inataka kuishtaki TFF itashinda na TFF
haitokuwemo FIFA kwani TFF haiwakilishi Tanzania kama ilivyokuwa ZFA
ilivyokuwa haiwakilishi Tanzania.
Hivi hatuoni haya kubakia hivi hivi kuwa Manispaa wakati Zanzibar
ilikuwa Empire alihoji Mwanasheria Mkuu na kuendelea kusema hivi
tutamuamini vipi mtu ambae leo anasema Zanzibar si Nchi atakapokuwa Rais
wa Tanzania ambao Zanzibar haitokuwa na Mamlaka atasema Zanzibar ni
jimbo la Tanganyika na kumalizia kusema wengi wa Watanganyika wanachuki
na Zanzibar.
Aliwataka wanafunzi hao kuzungumzia mambo ya Muungano na kutaka kuwe
na usawa “Bila ya kuwa na usawa katika Mungano huu huo si Muungano bali
ni ukoloni” alisema, na kutaka kuwe na mfumo wa usawa katika Baraza la
Mawaziri na Bunge na kuwe na makubaliano ya thuluthi mbili kila upande
katika kupitisha sheria na kuengezwa au kupunguzwa mambo ya Muungano.
Alisema katika Muungano wa Serikali Tatu ni lazima Rasilimali
zitumike kwa Usawa na sio kama hivi sasa Tanganyika inavyotumia
Rasilimali za Muungano wao peke yao katika kusoma na kuinyima Zanzibar.
Tume ya Pamoja ya Fedha haijaanza kazi mpaka leo, na katika Muungano
kuna mapato ya Muungano na Matumizi ya Muungano na Mapato ya Muungano
siku zote huwa mengi ambako Tnganyika hawataki tugawane.
Alisema si kweli kama Muungano wa Serikali tatu una harama bali
Muungano wa Serikali Mbili ndio wenye gharama na Zanzibar ndio
inaharamika zaidi, aliwataka viongozi wawe wakweli na waache kuwapotosha
wananchi.
Aliwaonya Wazanzibar kuwacha kulumbana na badala yake kukaa pamoja kuidai nchi yao.
Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliundwa ili kuondowa tofauti
kwa Wazanibar na kusema kuwa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni
kuala gumu kuliko mabadiliko ya Muungano.
Alisema Wanaotaka Seriakali Mbili hoja zao hazina msingi na hakuna
haja ya kubakia kwenye Serikali mbili na wengi wanaotaka Serikali Mbili
wanalinda maslahi yao ya kidunia.
Hoja yangu nawataka wanaotaka Serikali Mbili na Wanaotaka Mkataba
wakae pamoja wajadiliano Mfumo wa Muungano wa Serikali Tatu mfumo ambao
utakuwa na Mslahi na Zanzibar.
Awali Mwenyekiti wa ZAHILFE alikanusha taasisi yake kuandaa kungamano
la tarehe 6 mwezi wa 7 lililofanyika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za
Kingeni na badala yake kongamano hilo liliandaliwa na Mkowa wa Wanafunzi
wa Vyuo Vikuu vywa CCM na kusema Taasisi yake haina mafungamano na
chama chochote cha siasa.
Kongamano hilo lilianza na Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na lilihudhuriwa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Marais 10 wa Serikali za Wanafunzi waliochangia katika Kongamano hilo
walitaka Zanzibar yenye Mamlaka Kamili na Usawa Katika Muungano
0 comments: