WA B U N G E wameazimia k u j i t a z a m
a kuhakikisha mbunge hatajwi kwa rushwa wala uvunjifu wa maadili na
Bunge linakuwa safi kabla ya kunyooshea vidole wengine.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema
azimio hilo limepitishwa na wabunge mjini hapa, kuwezesha Bunge
kujitakasa na kuwa mfano wa kupambana na rushwa nchini. Kwa mujibu wa
Ndugai, suala la maadili kwa wabunge, viongozi wa serikali na wa dini ni
changamoto kubwa inayolikabili taifa.
Alisema hayo jana wakati akifunga
mafunzo ya wiki moja kwa wabunge, ambao ni wajumbe wa Kamati za
kusimamia fedha za umma na Bajeti, mjini Bagamoyo.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Ofisi ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Katika mafunzo
hayo, ambayo Naibu Spika pia alikuwa mshiriki, alisema suala la maadili
na rushwa limezungumzwa na kujadiliwa kwa kina na kubaini kuwa ni tatizo
kubwa nchini.
Alisema, “tumeona kabla ya Bunge
kunyooshea wengine vidole, linapaswa lijitazame lenyewe na kuwa safi kwa
kuhakikisha wabunge hawatajwi kwa rushwa na uvunjifu wa maadili kwa
kuwa wao ni mfano kwa jamii.
Alisema, “Maadili ni eneo lenye matatizo
mapana ndani ya nchi, sote tunahusika, wabunge wameona wazi huwezi
kupambana na rushwa kama huna maadili, ni wito na azimio la wabunge hapa
kwamba juhudi zianzie katika familia, lakini pia hata bungeni sisi
wenyewe tunapaswa kujitazama kwanza tusitajwe kwa hili, ili
tulisimamie.”
Ndugai pia alisema ni mapendekezo ya
bunge kubadili mfumo wa ukaguzi wa hesabu za serikali na ufuatiliaji wa
kamati unaofanyika baada ya fedha kutumika na kutumia pamoja na huo wa
jumuiya ya madola, ule wa Bunge la Marekani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: