NA HII NDIO KAULI YA WAZIRI WA CCM ILIYOZUA KIZAA ZAA JANA BUNGENI LIVE


Naibu Katibu wa Fedha, Mwigulu Nchemba  jana  katika Bunge Maalum La Katiba alichafua hali ya hewa baada ya kumwambia Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa kwamba wanataka wabunge wa bunge hilo watumie kura ya siri badala ya wazi kwa kuwa ni mashoga.

"Wanaotetea kura ya siri itumike katika kupitisha Katiba ya Watanzania, wanaunga mkono sera za ushoga, ni wale ambao vyama vyao vinazaminiwa na wanaotetea sera za ushioga," alisema Nchemba bungeni.

Kutokana na Kauli ya Nchemba, bunge hilo lilipuka likitaka aombe radhi huku akionyesha kusita kuomba radhi, lakini Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan alimtaka aombe radhi mara kadhaa.

"Mheshimiwa Mwigulu, naomba usimame na kuomba radhi wabunge wenzako, tafadhali simama," alisema Samia

Baada ya kauli ya Makamu Mwenyekiti Samia, Mwigulu alisimama na kusema: "Mheshimwa Makamu Mwenyekiti, Naomba radhi kwa wote wanaodhani wao wako hivyo kama nilivyosema."

Kauli hiyo ilionekana kuendelea kuwachefua wabunge wa bunge hilo huku wakimzomea na kumtaka aombe radhi kwa kuwa bado alikuwa hajaomba radhi moja kwa moja bali kauli yake ilionekana kuwa na utata.

Kwa mara nyingine, Makamu Mwenyekiti, Samia alisimama tena na kumtaka aombe radhi. "Mheshimiwa Mwigulu tafadhali omba radhi bila condition, tafadhali, bila kuomba radhi, Bunge haliwezi kuendela, na ninyi wabunge wengine kaeni kimya bila utulivu hatuwezi kusikilizana, tafadhali," alisema Samia.

Baada ya kauli kauli ya Makamu Mwenyekiti, Samia, Mwigulu alisimama tena na kuomba radhi kwa heshima na bunge kuendelea na utaratibu wake.

"Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti, nakiheshimu hicho kiti hapo mbele, siwezi kudharau, Naomba radhi kwa wote nilowaudhi," alisema Mwigukulu na kukaa chini.

Baada ya kauli ya Mwigulu ya kuomba radhi, shughuli za bunge ziliendelea kama kawaida
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: