AIBU:SHAROBARO AFUMWA LIVE AKILA URODA NA MKE WA MTU NDANI YA GARI BOVU


Arobaini (40) za mke wa mtu zimetimia baada ya kunaswa ndani ya gari akifanya uzinifu na kijana mmoja mtanashati ‘Sharobaro’ aliyejitambulisha kwa jina la Athumani (26) maeneo ya Bamaga Mwenge, jijini Dar.
 Tukio hilo lilitokea usiku wa manane Februari 4, baada ya mke  huyo aliyetambulika kwa  jina moja la Husna na sharobaro wake kujiingiza kwenye mtego na kunasa wazimawazima.
Mara baada ya kunaswa na kutakiwa kuvaa nguo zao, Sharobaro aliomba asipelekwe polisi na kuapa kutorudia tena huku akimtupia lawama zote mwanamke aliyekuwa naye.
 
Naye mwanamke huyo alisema kuwa kukamatwa kwake ni kama ajali kazini kwa kuwa tangu aanze biashara hiyo amekamatwa mara nyingi lakini si katika mazingira kama hayo.
“Jamani nimekamatwa mara nyingi sana lakini siyo katika mazingira ya aibu kama haya, hata mwenyewe sijapenda,” alisema mwanamke huyo.
 
Hatimaye wote wawili walichukuliwa na polisi na kupelekwa kituoni na  kufunguliwa jalada la kesi KJM/RB/ 1081/2014.
  
 Hata hivyo, taarifa tulizozipata wakati tukienda mitamboni kutoka kwa msichana anayedaiwa pia ni changudoa zilidai kuwa, mwanamke huyo ni mke wa mtu na amekuwa akiingia ‘viwanja’ mumewe akiwa nje ya Jiji la Dar.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: