INASIKITISHA:AKUTWA AMEJINYONGA MPAKA KUFA JUU YA MTI -UGUMU WA MAISHA NDIO SABABU
Mtu
mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Bahati maarufu kwa uuzaji wa
mifuko ya plastiki maeneo ya stand kuu ya mabasi Bukoba amekutwa
kajinyonga juu ya mti maeneo ya ufukwe wa Spice Motel majira ya saa
nane mchana ..
Taarifa
za awali kutoka kwa watu waliokuwa katika tukio hilo zinasema kuwa ,
kabla ya kifo cha, marehemu alionekana akiwa na mafurushi ya vitu na
alikuwa akifua katika eneo hilo la ufukwe…
Mtu
mmoja ambae hakuwa tayari kutaja jina lake ameueleza mtandao huu
kuwa leo majira ya saa 12.00asubuhi alisalimiana na marehemu maeneo ya
stand ya mabasi akiendelea na shughuli yake ya kutembeza mifuko ya
plastiki kwenye mabasi yaendayo mikoani na maeneo mengine akiwa mzima
wa afya.
Mwili wa marehemu umepelekwa Hospital ya Mkoa wa Kagera kuifadhiwa kwa ajili ya utambuzi ( ndugu zake )
Askari akiwa amepanda mti ili aweze kukata kamba aliyotumia kujinyonga
Amekutwa katika hali hii
Haijafahamika ni kwa nini kachukua maamuzi haya
Mwili wa marehemu ukishushwa
Kamanda wa polisi wilaya ya Bukoba akishuhudia tukio
Wananchi waliokusanyika katika tukio
Mkuu wa kituo cha polisi Bukoba(mwenye koti) akiwa anaangalia baadhi uya vitu vya marehemu alivyokuja navyo kabla ya kujinyonga
Hivi ni vitu vya marehemu alivyokuja navyo babla ya kujinyonga
Maeneo ya spice beach
Mmoja wa watu wa kwanza kutoa taarifa kituo cha polisi Mama Faima
Mwili wa marehemu ukipakiwa kwenye gari la polisi
0 comments: