Actress Yobnesh Yusuph(Batuli) yupo katika mikakati ya kuajiri meneja
ambaye atafanya nae kazi kitaalam zaidi na sio meneja wa kukaa naye na
kunywa pombe kwa mujibu wake mwenyewe. Pia muigizaji huyo yupo katika
mikakati ya kurudi shule ili kuongeza elimu yake ikiwa ni moja ya
malengo yake ya kufika mbali zaidi katika kazi zake za filamu. "Ili
nifike mbali lazima nisome, lazima niongeze taaluma yangu" alisema
muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto. Pia Batuli anatarajiwa kufanya
project flani na wasanii zaidi ya watano wa kimataifa hivi karibuni
hivyo muda ukifika utawajua hapa hapa SWP.
|
0 comments: