AFISA UTUMISHI WA MANISPAA YA ILEMELA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA YA NGONO ...
Afisa
utumishi wa manispaa ya Ilemela ndugu Songoma leo amefikishwa
mahakamani akikabiliwa na kesi ya rushwa ya ngono kwa mwalimu
aliyekuwa akiomba kuhamishwa toka Ngudu kuja Mwanza.
Akisomewa shitaka lake mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Mwanza, ofisa
wa TAKUKURU Bi. Debora amedai kuwa Songoma alitenda kosa hilo
may tano mwaka jana ambapo maofisa wa TAKUKURU walifanikiwa
kumtia mbaroni wakati akijiandaa kupokea rushwa ya ngono ndani
ya gesti moja jijini mwanza katika mtego ambao uliandaliwa na
mwalimu huyo.
Hata hivyo, Afisa huyo amekana shitaka hilo na kesi yake imeahirishwa hadi septemba 13 mwaka huu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: