LAANA..!!. MAMA NA MTOTO WAPEANA MIMBA KWA MARA YA PILI..
Kijana
mmoja nchini zimbabwe katika kijiji cha pote amekimbia kijiji hicho
baada ya kujikuta katika matatizo makubwa kufuatia kumtia mimba mama
yake mzazi kwa mara ya pili.
Ikumbukwe hapo nyuma kijana huyo aliwahi
kutenda kitendo hicho ambapo wana kijiji walimsihi kutorudia tena
kitendo hicho baada ya kijana huyo kumshawishi mama yake na kuitoa mimba
hiyo.
Simon Matsvara na mama yake Ethel Vhangare aliamua kuondoka baada ya waumini wa kanisa lao kugundua kuwa mimba hiyo ni batili.
Miaka minne iliyopita, wawili hao waliripotiwa na kutozwa faini na viongozi wa kijiji kwa kosa la kutoa mimba.
Chifu wa kijiji, Chinamhora alisema kuwa
jamii ilikasirishwa na kitendo hicho na kwamba yeye aliamua kuwatuma
wafanyakazi wake kuwatafuta wawili hao waliokuwa wameamua kuishi kama
mume na mke.
“Tunaenda kuwatafuta mpaka tuwapate na
wakisha patikana ni lazima wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu
wengine wanoa jihusisha na vitendo kama hivyo ambavyo havikubaliki
katika jamii”Alisema chifu huyo.
Imeripotiwa kuwa wawili hao walianza
mahusiano yao tangu mwaka 2008 wakati Matsvara alipopewa jukumu la
kumuuguza baba yake mzazi mzee Agripah,ambae baadae alikufa.
Mama huyo alipata mimba mara ya kwanza, wawili hao walitozwa faini na kuambiwa uhusiano wao ukomee hapo wasije wakarudia tena.
Habari ya mimba ya pili ziligundulika
baada ya mama huyo kuanza kuwakwepa wahumini wa kanisa lake walipokuwa
wakimtembelea nyumbani kwake.Baada ya uchunguzi ndipo walipogundua kuwa
mama huyo ni mjamzito wa miezi 5 na ujauzito huo kapewa na mwanae.
“Wawili hao wameamua kukimbia kijiji chao baada ya kugundulika wamejihusisha na kitendo hicho.”
0 comments: