SOMA BAADHI YA MIPASHO NDANI YA BUNGE LA KATIBA
ULIFANIKIWA KUSIKIA MIPASHO NDANI YA BUNGE LA KATIBA JANA (14/4/2014)? KAMA ULIKOSA SOMA HAPA USOME BAADHI YA MIPASHO ILIYOJILI.....
Haya ni maneno yaliyosemwa na baadhi ya wajumbe wa bunge maalumu la katiba leo tarehe 14 Aprili 2014.
Tanganyika ikirudi itazaa jamhuri ya Makonde, Nyamwezi!
Mbona Comoros haijawa Hong Kong?
Unadai cheti cha kuzaliwa cha baba yako ili iweje?
Mtu anayefanya mambo kipekeyake anaitwa mchawi!
Nyerere alikufa akiwa mwana CCM na alikufa akiwa ahajabadili msimamo wake, lakini alifariki baada ya tume zote kufanya mambo yake!
Kero za muungano zitamalizwa na taratibu mtakazoziweka....na mkishindwa kusikilizana wageukieni viongozi wa dini, mfano, Pengo alisema Serikali mbili zinatosha!
Tunaomba rasirimali zirudi mikononi mwa wananchi.
Kaa kitako, mjinga tu (imesikika kwa pembeni).
Zanzibar ni nchi na JK anajua hilo. Ndiyo maana alipoenda kwenye sherehe za mapinduzi alikaa na akamsubiri mwenye nchi. Na katika kuondoka aliondoka kwanza Rais wa wa Znzibar mwenye nchi.
Hamna lolote...mnaogopa gharama nyie kweli? Mbona mmeweka mawaziri mpaka wasio na wizara maalumu?
0 comments: