KUFURU:MAPOLISI DUBAI HUTUMIA LAMBORGINI NA FERRARI KUFANYA DORIA
Amini
usiamini brand za magari zilizojaa katika garage ya polisi ya Dubai ni
Lamborgini, McLaren MP4-12C, Aston Martin, Ferrari, Bentley na
Chevrolet.
Mwaka jana tuliwahi kuandika kuhusu chuo cha Dubai ‘American University in Dubai’ chenyewanafunzi wengi wanaomiliki magari ya kifahari duniani, lakini sasa ni polisi wa Dubai ambao wamenunuliwa magari hayo kwaajili ya kufanya patrol za kawaida mitaani.
Hata maaskari wenyewe wa Dubai wamekiri kuchanganyikiwa baada ya kupewa magari hayo kwaajili ya kufanyia kazi.
Mmoja wa askari hao aitwaye Mariam Ahmed, ambaye binafsi anamiliki
Toyota Land Cruiser amesema alipokabidhiwa kuendesha Ferrari FF kwaajili
ya doria mitaani hakuamini, na huwa anatamani asipate Off awe kazini
muda wote sababu ana enjoy kuwa kwenye Lamborgini awapo zamu.
“Ni mara yangu ya kwanza kuendesha Sport car”, alisema “waliponichagua
sikuamini, ni raha sana kuiendesha, nikiwa off huwa naimiss sana siwezi
kuifananisha na Land Cruiser yangu”.
Aliongeza, “inafurahisha sababu kuna watu huwa wanatuomba tuwakamate kwa
sababu yoyote ya kubambikiza ili tu wapande Ferrari wakati wa kwenda
polisi”.
Askari mwingine aitwaye Abdullah Mohammed , alisema magari hayo yamewaongezea ujiko wanapokuwa wanayaendesha mitaani.
“Kinachofurahisha zaidi katika kuendesha gari kama hiyo ya kifahari ni jinsi watu wanavyokutazama na tabasamu kubwa”.
Kwa mujibu wa GeeksTopten Dubai
ndio inakamata nafasi ya kwanza katika Top 10 ya nchi zinazoongoza kwa
kuwa na magari ya polisi ya gharama zaidi 2014, ‘Top 10 Countries Having
Most Expensive Police Cars in 2014’.
0 comments: