UKAWA RUDINI BUNGENI JAMANI TUENDELEE KUPATA UKWELI NA VIOJA
Kutokana na Bunge kupwaya sana baada ya UKAWA kutoka,ninawaomba warejee Mjengoni ili waendelee kutupa elimu ya Uraia ambayo tulikuwa tunaipata wakati session ikiendelea na sasa hatuipati.Tunaelewa kabisa kutoka na idadi yao kuwa ndogo mle ndani ni dhahiri kuwa hawawezi kushinda,lakini mioyoni mwa Watanganyika waliowengi nje ya jengo na Wazanzibari,hakika katiba hiyo haitapigiwa kura kutokana na halihalisi ya Rasimu ya Tume ya Warioba kuchakachuliwa.
Hivyo basi,Nawaomba kuwasihi warejee mjengoni ili kukamilisha hatua hii ya Bunge la Katiba na kuendelea na kasi ileile ambayo inatusaidia sana Wajumbe tulio nje ya Jengo kufunguka na kupata uelewa halisi wa swala lenyewe.

0 comments: