Showing posts with label MAKALA. Show all posts

GARI LA GURUMO ALILO PEWA NA DIAMOND LAZUA UTATA KWENYE FAMILIA

0 comments

AMA kweli asiyekuwepo na lake halipo! Lile gari la aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyefariki dunia hivi karibuni, Muhidin ‘Maalim’ Gurumo alilopewa na nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeibua utata mtupu ndani ya familia ya marehemu huyo baada ya kubainika kwamba kumbe hakupewa kadi yake

Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka ndani ya familia hiyo jambo hilo lilifahamika kufuatia mgogoro mkubwa unaoendelea kufukuta miongoni mwa wanandugu hao ambao sasa wamechangukana kutokana na mgawanyo wa mali za marehemu.
Ilijulikanaje kama hakuna kadi?
Chanzo hicho kilimtaja mtoto wa kike wa marehemu Gurumo aitwaye Mariam ambaye anataka nyumba na gari hilo aina ya Toyota FunCargo viuzwe ili watoto wagawane fedha.

“Yule binti alikwenda nyumbani kwa mama yake (mke wa mwisho wa mzee Gurumo aliyekuwa akiishi naye kwenye nyumba yake Mabibo, Dar) na kumtaka ampe kadi ya gari akidai ni la kwake na anataka kuliuza.
“Mama mtu alimwambia mwanaye kuwa baba yao hakupewa kadi hiyo siku alipokabidhiwa gari hilo.
“Hata hivyo, mama huyo alisema siku moja mzee Gurumo alimfuata Diamond alipokuwa akifanya shoo pale Coco Beach (Dar) kwa ajili ya kuulizia kadi hiyo ndipo Diamond akamwambia kwamba akitaka kadi amuulize mtu mmoja aliyesema ni kiongozi mmoja, anafanya kazi maeneo ya Posta Mpya jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa),” kilisema chanzo.


Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya Gurumo kuambiwa maneno hayo, hakutoa jibu lolote kwa mke wake kama alipewa kadi hiyo au la, lakini mama huyo hakuwahi kuiona.
Kukosekana kwa kadi hiyo kumesababisha kuendelea kuwepo kwa gari hilo, kwani kama ingekuwepo, lingeshauzwa.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Diamond zilisema kuwa tukio la kutoa gari kwa mkongwe huyo mwanzilishi wa Bendi za  Mlimani Park Orchestra na Msondo Music Band ulikuwa ni mpango maalum wa kumpromoti msanii huyo ili aweze kung’ara zaidi katika vyombo vya habari ambao uliratibiwa na kiongozi huyo mwenye kulalamikiwa na wasanii mara kwa mara

Soma Zaidi»

SABABU YA MAREHEMU GURUMO KUPOTEZA JICHO LAKE MOJA HII HAPA

0 comments

Marehemu Gurumo kwa maisha yake yote alikuwa na ulemavu wa jicho moja lakini hakuna mwanamuziki wala mdau  au mwanahabari aliyekuwa anajua sababu ya madhila hayo ya mzee wetu mpendwa.

Gurumo akaileza Saluti5 mbele ya mdau mkubwa wa muziki Juma Mbizo sababu ya jicho lake kupotea.

Ilikuwa jambo la kusisimua sana. Alitupeleka hadi mbele ya nyumba yake na kukutana na mti wa mwembe na kisha akasema: “Leo nataka niwaambie jambo moja ambalo sijui kama yupo mtu anayelijua.

“Huu mti una historia kubwa kwangu. Hapa ndipo nilipopoteza jicho langu nikiwa na umri wa miezi mitatu.

“Mama yangu alinilaza kwenye kivuli cha mti huu kisha akaenda kuendelea na shughuli zake. Bahati mbaya likaanguka tawi na kutua kwenye jicho langu.

“Nilisimuliwa kuwa juhudi za hospitali hazikusaidia kitu, nikapoteza jicho langu,” alimaliza Gurumo na kisha akataka arekodiwe kwa njia ya video ili tujipatie kumbukumbu adimu.
Baadae tutakuwekea video ya Gurumo akisimulia namna alivyopoteza jicho lake.

Soma Zaidi»

MPOTO AELEZA SABABU ZA YEYE KUTEMBEA BILA VIATU HATA AKIENDA ULAYA

0 comments

Msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto amedai kuwa ajisikii vizuri pindi anapo vaa viatu kutokana kudai kuvaa viatu kuna athiri utendaji wa kazi zake.

Mpoto ameiambia bongo5 kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika.

“Beauty yoyote ipo kwenye jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy ,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana kwenye udongo,yani ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto, zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu navaaga kwasababu watu wananisema.kwaiyo nikivaa ninakuwa kama inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo kwangu mimi ardhi ni kama plug ya mwili wangu,nikikanyaga chini wewe niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la michanga,kwajili tu yakukanyaga yani nikiandika nakuwa confidant ata nikiandika nakuwa na amani”Alisema Mpoto

Pia Mrisho ataendelea kufafanua kwanini ataki kubadilika na kuchana na tamaduni ya kutembea mbila kuvaa viatu

“Nataka maisha yasiniendeshe mimi,mimi niyaendeshe maisha, kwasababu unajua speed ya utandawazi yani globalization ni kubwa sana kuliko speed ya mwanadamu kwa Tanzania,ukiangalia watu kama Marekani wamepata uhuru miaka mia mbili iliyopita,sisi tuna miaka mingapi tu ya uhuru na teknologia inakuja kwa kasi sana,ndiyo maana technologia inapokuta Tanzania watu wanaimasta sana,kwamfano facebook,instargam,twetter,whatsapp na mitandao mingine vimekuja kwa kasi sana na watu vimewabadilisha sana,ata Ngugi wa Thiong’o alisema huwezi kwenda kwa jirani kama ujatokea kwako,mtu kaka mimi ninapoigia kwenye technologia siwezi badilishwa kwasababu nimeshajijua mimi ni
nani”Alimalizia Mpoto

Soma Zaidi»

MASAI NYOTAMBOFU AJIONDOA KWENYE KUNDI LA VITUKO SHOW, SOMA KISA KIZIMA HAPA

0 comments


MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini katika swaga za kimasai ambaye pia ni mmiliki wa masainyotambofu.info Gilliady Severine Kahema 'Masai Nyotambofu' Ameamua kuitema kampuni aliyokuwa na mkataba nayo ya Al-Riyamy Pro ambayo hurusha kipindi chake cha VITUKO SHOW kwenye runinga ya CHANNEL TEN. 
Akizungumza  leo, Masai Nyotambofu alisema kuwa ameamua kuachana na kampuni hio baada kugundua kuwa kuendelea kuwepo pale kwa muda mrefu ni sawasawa na kuididimiza sanaa yake kwani hamna mafanikio yeyote zaidi ya kuahidiwa kwamba baada ya kipindi fulani mambo yatakuwa mazuri huku siku zinazidi kwenda, ''Kiukweli nimeamua kuachana na Al-Riyamy Pro maana naona muda wote wa miaka mitano sijafikia malengo yangu niliotarajia na ahadi za kampuni hazionekani,

Pia kikubwa zaidi kilichoniondoa ni pamoja na kuchezeshwa na wasanii wasio na vipaji halisi wanaishia kuigaiga stile za watu tu hatima yake tunaonekana wote wabovu. Hapo mwanzo tulivyokuwa timu kamili tulifanya vizuri na kupokelewa vizuri lakini walivyoondoka baadhi ya wasanii wenye uwezo mkurugenzi akasema analeta wasanii wengine, Basi mimi nikaendelea kusubiri maana kila msanii alikuwa na mkataba wake hivyo kila aliyeondoka aliondoka kwa sababu zake binafsi mimi nikaendelea kukomaa nikihisi mbele ya safari kutakuwa na mabadiliko, Mara mkurugenzi akaaza kuwaleta watu tu from no whwre wasio na vipaji vya sanaa tucheze nao, Kila nikimuuliza kuwa mbona wengine wakisimama mbele ya Camera wakiambiwa Action hawajui itakuwaje? Jibu lake alinijibu nawasaidia maisha yao magumu. Nikamwambia huoni kuwa kazi ikiwa mbovu tutapoteza mashabiki? Akajibu we fanya kazi ntapitisha mchujo wasio na vipaji ntawaondoa watabaki wenye vipaji wachache tu niwatengenezee maisha ili muuone umuhimu wa kukaa kwenu hapa miaka mingi mimi nauona uvumilivu wenu, Cha ajabu mkurugenzi aliendea kujaza watu wasio na vipaji uongozi hakuna nidhamu kambini mbovu mimi siheshimiwi na mimi simuheshimu mtu basi tafrani kama kilabu cha komoni. Lakini nikaendelea kukomaa nikitarajia mabadiliko mwaka 2014, Kuna siku nikajaribu kumwambia mkurugenzi kuwa aniazime kiasi fulani cha fedha nikamilishe Video ya wimbo wangu alafu anikate akasema sina hela huoni mko wengi? kwanza kampuni hainilipi wewe unataka upate promo ili uzidi kuitwa kwenye Show utashuti saa ngapi na kwenye Show utaenda saa ngapi? Dah! Hapo ndipo nilipoona kuwa napoteza muda ukizingatia mwanzoni tulivyokuwa wakali watupu kipindi kikiruka hewani simu za wasanii zinaita mpaka kero lakini sasahivi kipindi kinaruka mwanzo mwisho hata hubipiwi..! Ni ishara tosha kwamba watazamaji wameanza kuingia mitini. Ni bora nikae pembeni nikinusuru kipaji changu kwani kama riziki yangu mwenyezi mungu hakuniandikia kuipata hapo hata nikomae vipi kamwe sitofanikiwa hapo. Nimeamua kurudi Nyumbani Jijini Dar kutuliza kichwa sina mkataba na kampuni yeyote kwa sasa najiandaa kuachia ngoma mpya baada ile niliyomshirikisha Rich Mavoko na Kitokololo (Yero Masai) Watu wangu kaeni mkao wa kula Uchekeshaji siachi mpaka mwisho wa uhai wangu, Kuondoka Al-Riyamy Pro Sio mwisho wa kampuni kufanya kazi wataendea wengine na wala sio mwisho wangu wa kuchekesha bado mtaendela kuzipata ladha zangu kupitia filamu zangu ambazo nipo katika mikakati ya kuanzisha Project. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa kipaji hiki kilichonifanya niwe na ukaribu wa hali ya juu na watu mbali mbali na katika show zangu napokelewa vizuri hicho kinanifanya nimuheshimu kila mtu wa kila rika, Nawapenda Mashabiki wangu One Love.

Soma Zaidi»

UKAWA RUDINI BUNGENI JAMANI TUENDELEE KUPATA UKWELI NA VIOJA

0 comments


Kutokana na Bunge kupwaya sana baada ya UKAWA kutoka,ninawaomba warejee Mjengoni ili waendelee kutupa elimu ya Uraia ambayo tulikuwa tunaipata wakati session ikiendelea na sasa hatuipati.Tunaelewa kabisa kutoka na idadi yao kuwa ndogo mle ndani ni dhahiri kuwa hawawezi kushinda,lakini mioyoni mwa Watanganyika waliowengi nje ya jengo na Wazanzibari,hakika katiba hiyo haitapigiwa kura kutokana na halihalisi ya Rasimu ya Tume ya Warioba kuchakachuliwa.
Hivyo basi,Nawaomba  kuwasihi warejee mjengoni ili kukamilisha hatua hii ya Bunge la Katiba na kuendelea na kasi ileile ambayo inatusaidia sana Wajumbe tulio nje ya Jengo kufunguka na kupata uelewa halisi wa swala lenyewe.

Soma Zaidi»

DARAJA LA DAR BAGAMOYO BADO SANA -MKONDO WA MAJI WABADILIKA

0 comments





Kazi katika Daraja la Mpiji lililoko Mpakani mwa Dar na Bagamoyo bado ni kubwa hizi ni picha za asubuhi hii Bado wanaendelea kumwaga mawe na kifusi lakini kazi inaonekana bado ni kubwa.....Daraja lenyewe alijavunjika kilichotokea ni maji yameacha mkondo wake wa kupita chini ya daraja na kuchimbua pembeni ya daraja ambapo kuna muunganiko wa daraja na lami ....Ukiangalia picha ya Pili na ya Tatu Inaonesha Skaveta likijaribu kuchimba chini ya daraja ili kuurudisha mkondo katika njia yake ya kawaida,,,,,Ni Shida....

Soma Zaidi»

MUHIDIN GURUMO (ALIYEKUWA MSONDO NGOMA) AFARIKI DUNIA

0 comments


Muhidin Gurumo (aliyekuwa Msondo Ngoma) afariki dunia!

Habari za hivi punde zinasema kuwa Nguli wa mziki wa bance Mzee wetu Muhidim Ngurumo amefariki dunia mchana siku hii ya leo.

Pole ziwafikie wapenzi wote na mashabiki!!


R.I.P Gurumo.
Chanzo.Uhuru Fm

Soma Zaidi»

JINSI MAFURIKO YANAVYOLITESA JIJI LA DAR..ANGALIA PICHA

0 comments

Mburahati na Mayfair leo asubuhi

Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira.

Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika na mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi hasa wanaoishi bondeni au kwenye mkondo wa maji mfano mito.

Soma Zaidi»

KAMA BADO UNATUMIA WINDOW XP KWENYE COMPUTER YAKO HII HABARI INAKUHUSU

0 comments
Are you still using Windows XP as your operating system? From today Microsoft will no longer offer support their operating system Windows XP. I am one of those culprits who have refused to upgrade because I feel this is not a change I need when I considering my PC uses. This will also mean I will have to say goodbye to a laptop I have had and become attached to since 2007 since it does not have the specs to upgrade to Windows 7 or 8.


So what does this mean exactly? from today if faults detected within the operating system, they will go unfixed.Banks are urged to upgrade their ATMs to a newer OS release as soon as possible as we know 95% of all banks in the world still use Windows XP. There has been efforts from the European banks to get continued support and they have a high price to pay as the UK government agreed to pay more than £5.6 million to Microsoft to continue its support for Windows XP by one year.

If you cannot move on and choose to remain on windows XP you have to ensure that you are protected do this by keeping away from Internet Explorer and use Chrome instead, have a strong antivirus in place, make sure the firewall is set and finally do not store personal information on the browser.
However there are benefits of upgrading for example you will notice that with the newer versions of Windows there are significant changes in the interface and vast improvements in the services available and the overall aim of this is to make the computer less of an appliance and more like a personal device, similar to a phone.

What will you do now that Windows XP won’t be supported by Microsoft? will you finally upgrade? or will you buy a mac or do you want to try linux? Share your resolutions with us.

Soma Zaidi»

IZZO BUSINESS ALIGOMA KUMPIGIA KAMPENI RIDHIWANI JAPO ALIOMBWA KUFANYA HIVYO

0 comments

Jumapili iliyopita (April 6), Ridhiwani Kikwete alitangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi wa kiti cha ubungo wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani.

Hii ilikuwa habari njema pia kwa Izzo Bizness ambaye aliwahi kumuimbia mbunge huyo ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete akimtaka aongee na ‘mshua’ kuhusu hali halisi ya mtaani.

Izzo Bizness ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa tangu atoe wimbo huo amekuwa karibu na Ridhiwani kimawasiliano na hata wakati wa kampenzi za ubunge wa jimbo la Chalinze alimuomba amsaidie lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ilivyokuwa kwa upande wake.

“Kuna vitu vidogo tu ambavyo tulipishana, niliangalia pia katika upande wangu. Hakikuwa kitu cha kusaidiana kimasihala kwa kuwa unapoamua kuingia kwenye kampeni kumsaidia mtu ujue ushaamua kutake risk. Na hapo mimi nilikuwa naenda kukipa tafu chama cha CCM lakini mimi natokea jimbo ambalo limeshikiliwa na CHADEMA na wananchi asilimia kubwa ni CHADEMA”. Amesema Izzo Bizness.

Source: Bongo5

Soma Zaidi»

MILIONI 13 ZAZUSHA TIMBWILI LA HATARII,WEMA NA KAJALA NGUMI NONDO NJE NJE WAPAMBE WAO WAINGILIA KATI.

0 comments

Stori: Imelda Mtema na Musa Mateja

NI shida! Zile shilingi milioni 13 alizotoa Wema Isaac Sepetu kumlipia msanii maarufu wa sinema Bongo, Kajala Masanja asitupwe gerezani, bado ni tatizo ikidaiwa kuwa sasa ngumi nje nje.
JINA LA MILIONI 13 ZA WEMA
Kwa muda mrefu sasa, Kajala amekuwa akitukanwa kwenye mitandao ya kijamii hasa matusi ambayo hayaandikiki huku akipachikwa jina la ‘Milioni 13 za Wema’ na kuahidiwa kichapo.
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Kajala, staa huyo hana raha wala furaha kwani ishu hiyo inamtesa kila kukicha.

Ilidaiwa kwamba Kajala ana mtoto mkubwa aitwaye Paula aliyezaa na prodyuza wa Bongo Records, Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye anajua kuingia kwenye mitandao hiyo hivyo kufedheheshwa hasa anapokuta mama yake akiitwa fuska wakati yeye anamheshimu.

KUNDI LA TEAMWEMA
Ilisemekana kwamba Wema ana kundi linalojiita TeamWema ambalo memba wake wamekuwa wakianzisha mada mbaya kuhusu Kajala wakimhusisha na uporaji wa aliyekuwa bwana wa Wema, Clement au CK.

Ilifahamika kwamba shinikizo kubwa la kundi hilo la Wema ni kutaka Kajala arejeshe fedha hizo ndipo mambo yakae sawa.

Soma Zaidi »

MAKOSA YA KAKOBE KUMWANDIKIA BARUA RAIS KIKWETE HAYA HAPA

0 comments


Wewe kama mtumishi wa Mungu hukutakiwa kuandika barua ikulu kwa sababu zifuatazo
kwanza kabisa kama mtumishi wa Mungu mzoefu ulitakiwa kukaa chini na kufikiri kabla ya kuandika
Pili unamuandikia barua mtu Ambae mna Imani tofauti  katika kufanya kazi zake
tatu unajaribu kupigana vita ya kimwili wakati watumishi wa Mungu mnatakiwa kupigana vita ya kiroho

wewe ni Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu sana,tangu nakua nasikia jina Kakabe,umekosea sana na imetokana na kiburi chako cha kutomshirikisha Mungu

ulitakiwa kufanya nini?
ulitakiwa kuongea na Mungu kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu
una uwezo mkubwa sana hapa duniani kuliko Kikwete na waliomzunguka
umeshindwa kujitambua kwamba una mamlaka wala huitaji kujiingiza kwenye upuuzi
una uwezo wa kukamata nguvu za giza anazotumia Kikwete wa wajinga wenzake kupitia ulimwengu wa Roho
ukifunga na kuomba na kumweka Kikwete mbele za Mungu ungeona matokeo
UNGEPATA NAFASI YA KWENDA BUNGENI UNGELETA MABADILIKO GANI?

Soma Zaidi»

LULU MICHAEL"JAMANI WASICHANA TUINUKE TUACHANE NA MAMBO YA KUHONGWA NA MATAJIRI"

0 comments


ELIZABETH Michael ‘Lulu’ amewaasa wasichana wenzake kujitahidi kujishugulisha na kazi mbalimbali kuingiza ‘chapaa’ na wasiendekeze kuhongwa fedha na mapedeshee kwani ni aibu.

Akistorisha na paparazi wetu pasipo kuweka wazi kama alishawahi kuhongwa au la, Lulu alitiririka:

“Jamani wasichana wote tuinuke tuachane na mambo ya kuhongwa fedha na matajiri kwani hizi zina mwisho wake, siku hizi mambo yote ni kujishughulisha.”

Soma Zaidi»

MZUNGU KICHAA AKANUSHA KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA SALAMA JABIR

0 comments

Msanii wa Denmark aliyeishi Tanzania muda mrefu, maarufu kama Mzungu Kichaa amezungumzia uvumi uliowahi kusambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha ‘Mkasi’, Salama Jabir.

Mzungu Kichaa amekanusha uvumi huo na kusema hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Salama. “Sio kweli mimi si-date na Salama Jabir” Alisema alipohojiwa na katika kipindi cha TV cha Sporah, “tulifanya kazi pamoja kama majaji katika kipindi cha TV (BSS), so kuna vitu vingi ambavyo tunafanana pia alisoma UK na ni mtu mzuri, so ni marafiki tu kulikuwa na uvumi ulisambaa kwenye media”.

alama Jabir Pamoja na kuwa hakuna ukweli wowote juu ya swala hilo lakini Mzungu Kichaa amedai kuwa kuna mtu aliwahi kumuuliza kama ana uhusiano na Salama na alimjibu ndio lakini hakumaanisha.

Mzungu Kichaa katika Sporah show “kuna mtu aliniuliza nikiwa uwanja wa ndege, Mzungu Kichaa ni kweli una uhusiano nae, ilinibidi niseme ndio kwasababu nilikuwa nacheka sababu ilikuwa ni idea ya kuchekesha kwamba Mzungu Kichaa ana uhusiano na Salama.” Alisema Mzungu Kichaa. Akiuzungumzia uhusiano wake na Salama amesema, “Sisi sio best friends so sio kwamba tunatoka sana pamoja, ninayo namba yake, na yeye lazima atakuwa nayo ya kwangu lakini hatutumiani ujumbe kila wakati.” Katika hali ya utani mzungu Kichaa alisema: “People thought it was really funny and they got excited about it because imagine if these two, the crazy white man and the crazy Salama, coz Salama is crazy imagine if those two have children how crazy they will be.” Aliongeza kuwa baada ya kusikia kinachozungumzwa mitaani aliwasiliana na Salama kumjulisha, “Nilimtumia barua pepe kumwambia kile kinachosemwa na watu ili asije kushtuka akija kusikia”. CREDIT : BONGO5

Soma Zaidi»

WAUMBUANA BUNGENI

0 comments


TABIA ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, hasa kutoka vyama vya upinzani waliounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutafuta kasoro ndogo ndogo za kutaka Bunge liahirishwe mara kwa mara, imewatokea puani. Jana baadhi ya wajumbe hao akiwepo Ismail Jussa Ladhu, Tundu Lisu, John Mnyika na Moses Machali, walisimama kupinga marekebisho ya kanuni za Bunge Maalumu kwa madai kuwa yameletwa haraka haraka na yana nia ovu.

Mtindo wao Alianza Jussa, akasema wajumbe hawana jedwali la marekebisho ya Kanuni hivyo ni bora hoja ya marekebisho hayo iahirishwe ili kuwapa nafasi ya kuyapitia na kuleta jedwali lao la marekebisho.

Wakati Jussa akidai wengi wao hawana jedwali hilo la marekebisho, alishangaa kuona wajumbe wenzake wengi, akiwemo aliyekaa naye wakipepea juu jedwali hilo, kuonesha ni yeye peke yake na baadhi ya wachache hawakuwa na jedwali husika kwa kuwa wengi walikuwa nayo.

Soma Zaidi »

PROF ISSA SHIVJI NA UBAKAJI WA MATAKWA YA UMMA KWENYE MUUNDO WA MUUNGANO

0 comments


Sijawahi kufundishwa na Profesa huyu anaeishi Amerika akighani sheria zake katika uga wa Pwani ya Azania, nimjenzi mzuri wa hoja za kisheria vilevile jamii ya kiswahili inamuamini kwa misimamo yake,


Baada ya Tanzania kuanza mchaato wa kupata katiba mpya ya Muungano, Prof Shivj alikuwa miongoni mwa watu wanaotazamiwa kulisaidia taifa kupata katiba bora kabisa ya "KIRAI", lakini katika hali isiyotegemeka, mamlaka zote za nchi zikamtelekeza, akawa sasa ni deiwaka tu msako wa katiba mpya, akionyesha kuheshimu misimamo ya uuma.

Mnyukano wa kimaslahi kati ya Chama cha Mapinduzi na UMMA wa Watanzania, umemrejesha tena Issa Shivji mbobevu wa sheria za kiutawala, lakini akija kwa nadharia ya kusigina matakwa ya umma,

Yule Issa Shivji aliyekuwa mtetezi wa matakwa ya umma, leo amekuwa mpiga zumari wa Lumumba. Issa Shivji anafikiri Watanzania ni wajinga kiasi cha kumfuata kila akifanyacho, vikao vyake vya ikulu wiki jana kwamalengo ya ghiriba wa umma havita saidia Watanzania kudai Muungano wao BORA kabisa wa Serikali TATU.


Hebu tujirejeshe kidogo kuitazama Nadharia ya Muungano.


Hoja za muudo wa serikali zinatafsiriwa na sababu kuu mbili ambazo ni hoja za kisheria na hasira za kisiasa.

1.HOJA ZA KISHERIA

Hoja za kisheria ni kwamba zinapoungana serikali mbili ni lazima pawepo na katiba ya serikali moja au tatu na wala sio mbili tena kisheria.Kwa mfano ni kwamba tume zote mbili zilizoundwa na Rais chini ya wasomi wa kisheria chini ya JAJI FRANSISI NYALALI na ile ya JAJI ROBERT KISANGA zote zilipendekeza serikali 3 na sio mbili.

Kwa mfano endapo utampa msomi wa kisheria kazi ya kukuandalia katiba ya serikali mbili zinazotakiwa kuungana atakuandalia katiba ya serikali ama 1 au 3 lakini sio mboli kwani hazipo kisheria.

2.HASIRA ZA KISIASA

Hasira za kisiasa ni sababu nyingine ya kuwa na serikali tatu,Kwa mfano mwaka 1984 aliyekuwa rais wa Zanzibar ABDU JUMBE aliasisi hoja ya kuwa na serikali 3 na ikamgharimu kunyang'anywa kadi ya CCM na kupoteza urais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na MZEE ALI HASAN MWINYI 1984-1985 kabla ya kuchukuliwa na IDRISA ABDUL WAKIL 1985-1990.

Mwaka 1993 paliibuka kundi la G55 liliokuwa na nia ya kuifufua Tanganyika kundi ambalo lilipelekea baraza la mawaziri kuvunjwa mwaka 1994 na baadhi ya mawaziri akiwemo waziri mkuu na makamu wa kwaza wa Rais kupoteza wadhifa wake.

Mwaka huo huo 1993 Zanzibar ilitaka kujiunga na OAC wakakataliwa kwamba hawana mamlaka ya kufanya hivyo ndipo aliyekuwa Rais wa wakati huo DR SALIMIN AMOUR JUMA akasema Zanzibar imedharauliwa na kuzidi kupandisha homa na hasira za Wazanzibar kudai mamlaka kamili ya Zanziabar.

Hata mwalimu Nyerere alikuwa na nia kwamba waunde serikali moja lakini kwa kuanzia alipendekeza kwamba waanze na serikali mbili ili wazanzibar wasiseme wamemezwa japo baadae alishindwa kuunda serikali moja.

Kwahiyo hizo ndio sababu za mkanganyiko uliopo Tanzania katika mchakato wa katiba mpya.

Soma Zaidi»

JE, MH. SITTA AMECHUJA AU AMEPAUKA?

0 comments


Alipokuwa spika wa bunge la 9,alitupa mwamko wa kufuatilia vikao vya bunge.Hasa pale aliporuhusu uundwaji wa kamati ya Mwakyembe iliyochunguza dili la richmond na hatimaye kupelekea kumwagika kwa unga wa EL.Wengi tulijua kuwa mzee amedhamilia kuleta mapinduzi ya kisiasa,kwamba hajali ni mtu wa chama gani,ila anachojali ni viwango na kasi.

Juzi ameaminika na kuchaguliwa kwa kishindo pale bungeni ili kuongoza bunge la katiba,akarudia katika maelezo yake kuwa atakuwa yule yule wa viwango na kasi,wengi wakampigia vigelegele,hata mimi nilifurahi na kurukaruka nikijua jembe limerudi shambani.

Ghafla,akatuacha solemba,akatuduwaza na kutuacha na mshangao mkubwa.Hii ilikuwa ni wiki jana pale alipokubali kanuni zisivunjwe ila zipindishwe.Ilikua amkaribishe JK aanze kuzindua bunge kisha afuatiwe na Warioba.Yeye 6,akapiga tiktaka akiwa amevaa taulo,akamleta kwanza Warioba ! Hii haikuwa kwa bahati mbaya,ila ilikuwa planned kabsaa! Yakawa yaliyokuwa na wote tumeshuhudia na kuhudhunika.Hivi kanuni walizojitungia zitafuatwa kweli kama wa kwanza kuzivunja ni 6 na rais wa nchi!?

Wadukuzi wa siasa zetu wanasema 6 alipewa shinikizo na chama chake ili aruhusu kwanza mwenyemeza wao(mwenyekiti) atanguliwe na Mzee Warioba ili baadae mwenyekiti aje kujibu mapigo.Vipi kama angetangulia mwenyekiti na kisha Warioba angefuata,je,mwenyekiti angesomeka kwa ile hotuba yake kweli?

Kwanini 6 anaonekana kuwa refa anayebeba timu fulani waziwazi? Mmeona kwenye kamati za uongozi alivyoteua?

Je, 6 amechuja au amepauka ?

Soma Zaidi»

DIAMOND AWACHANA BASSATA..BAADA YA KUONDOA NYIMBO KADHAA KATIKA KILL AWARDS

0 comments

Baada ya nyimboz ya SNURA (MAJANGA), TEMA MATE TUWA CHAPE ya MADEE na JUX (UZURI WAKO) kuondolewa katika KILI Awards hiki ndicho alicho kisema msani Nassib Abdul A.k.A DIAMOND PLATNUMZ…. 
“ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje… Hii ni sawa na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu… Will the target of reaching our goals ever be achieved?? #Ni_Mtazamo_tu” 


Soma Zaidi»

WASANII WAMWOMBA JK AWASAIDIE KUPATA HAKI ZAO NYIMBO/VIDEO ZINAPOCHEZWA KWENYE RADIO/TV

0 comments


Giza nene bado limetanda kwa wasanii kuhusu hakimiliki ya kazi zao kutokana na Chama  cha Hakimiliki Tanzania (Cosota), kukiri wazi kwamba wameshindwa kukusanya mirahaba ya wasanii kupitia vyombo vya matangazo, zikiwemo redio na televisheni, kutokana na kukosa mitambo ya kisasa ya kufuatilia kazi hizo.

Vyombo hivi vya matangazo vimeshindwa kuwalipa wasanii, lakini hivi sasa vimekuwa vikiongoza kuwatoza wasanii fedha ili kazi zao zipate kusikika redioni au video zao kuonekana hadharani. Hata hivyo, wasanii nao wamekuwa wakilipia fedha nyingi ili  nyimbo zao zipigwe na kufahamika kwa mashabiki, kwa lengo la kupata shoo ambazo ndiyo malipo ya kazi zao.

Kinachowaingizia fedha wasanii wa sasa ni kupitia shoo, mfumo ambao umekuwa ni ‘mama’ katika mataifa mengi duniani. Shoo ndiyo msingi pekee kwa msanii, hii inamaanisha nini?

Iwapo msanii atachuja na nyimbo zake kuendelea kupigwa redioni na hata video zake kuendelea kuchezwa kwenye vituo vya televisheni, inamaanisha kwamba hatakuwa na stahili yoyote anayoipata kupitia jasho lake, ilhali chombo cha habari husika kinaingia fedha kupitia matangazo mbalimbali.

Akizungumza na gazeti hili, Mwanasheria wa Cosota, Maureen Fondo Jandwa anasema mpaka sasa kuna kituo kimoja tu cha redio kilichopo mikoani, ndicho kinacholipa mirabaha kwa wasanii ambapo hata hivyo ni kiasi cha shilingi laki tano tu kwa mwaka.

“Licha ya kwamba Cosota hatuna mitambo ya kurekodi lakini sheria ya leseni kwa vyombo vya utangazaji wa kazi za wasanii ya mwaka 2003, imepitwa na wakati hivyo kwa sasa tunasubiri mchakato wa sheria mpya ili wasanii waweze kunufaika,” anasema Jandwa huku akifafanua kuwa wasanii wanalipwa mirabaha inayotokana na kazi mbalimbali zilizorekodiwa kupitia Juck Box na kwenye kumbi za starehe na bado kuna utata katika maonyesho ya umma na vyombo vya utangazaji.

Soma Zaidi »

HATIMAYE MBUNGE WA CCM EAST AFRICA APINGANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LAIVU BILA CHENGA

0 comments

Shy-Rose Bhanji

About an hour ago

As a Citizen & Patriot of my Motherland Tanzania, I give due respect to the opinions of all Tanzanians on the current Constitution review. 

Much as convictions and beliefs of President JK (2govts) and Judge Warioba (3govts) are divergent, I will support the popular decision thru the coming National referendum. 

However, for now, my stand is for 3 Governments because of the following:
1. The life-span and relevance of the two-tier Govts has reached its end.
2. Complaints/grievances on Union issues have not been solved for mutual benefit.
3. A 3tier govt is the ultimate solution given the 2 reasons above. And to me this an evolution of the reality...

Kama Mtanzania na Mzalendo, ninaheshimu mtazamo/mawazo ya Watanzania wote. 

Licha ya kwamba mawazo ya Rais JK (Serikali 2) na Jaji Warioba (Serikali 3) yametofautiana, binafsi nitaunga mkono hoja/msimamo wa wengi kupitia kura za maoni za kitaifa. 

Hata hivyo kwa sasa bado ninaunga mkono muundo wa Serikali 3 kwasababu zifuatazo:

1. Mfumo wa Serikali 2 unaonekana kufikia kikomo na kutokuwa na umuhimu tena baada ya miaka 50 ya uhai wake.
2. Kero za Muungano zimeshindwa kupata suluhisho/muafaka kwa manufaa ya wote.
3. Muundo wa Serikali 3 ndio jawabu pekee kwasababu nilizotoa hapo juu. Na kwangu mimi hatua hii ni muendelezo wa hali halisi...

Soma Zaidi»