MSIKITI WA ANSWAR SUNNA ULIOPO MJINI DODOMA WATEKETEA KWA MOTO...
Akiongea kwa njia ya simu na Mpekuzi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo...
Hata hivyo, shuhuda mwingine aliyeongea na mtandao huu amedai kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia ghorofa ya juu ya jengo hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na moto huo.
Tunaendelea kufuatilia undani wa tukio hili
0 comments: