HAYA NDIO MASHTAKA MATATU ALIYOSOMEWA WILLIAM RUTO MBELE YA MAHAKAMA YA ICC..
Haya ndo mashitaka matatu aliyosomewa makamu wa Rais wa Kenya mbele ya mahakama ya ICC
William Ruto amekana mashtaka yote yanayomkabili kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou
Bensouda anayesimamia kesi hiyo, alisema watuhumiwa wawili waliofikishwa
mahakamani hapo jana, Ruto na mtangazaji wa Redio, Joshua arap Sang
wanakabiliwa na mashtaka matatu kila mmoja, ambayo ni kuwalazimisha watu
kukimbia makazi yao, mauaji na kuchochea ghasia.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa siku chache baada ya
Bunge la Kenya kupiga kura kutaka nchi hiyo ijitoe uanachama wa ICC,
wakieleza kwamba imekuwa haina tija na inatumiwa kuwakandamiza Waafrika.
Ruto ambaye alionekana kujiamini alifika kwenye
jengo la Mahakama akiwa ameambatana na baadhi ya wabunge waliosafiri
kutoka Kenya hadi The Hague kwa ajili ya kumuunga mkono.
Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda alianza
kwa kusoma mashtaka matatu yanayomkabili kiongozi huyo wa Kenya na
akaiomba Mahakama hiyo kumtia hatiani kutokana na vurugu zilizojitokeza
baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Akiwasilisha hoja ya mashtaka, Bensouda alisema
kuwa Ruto ni mwanasiasa aliyejawa na kiu ya madaraka na wakati fulani
aliitii kiu yake kwa gharama ya maisha ya wengine.
Alieleza kuwa Ruto alianzisha machafuko alipoona shabaha yake kutwaa madaraka kwa njia ya kura kushindwa.
Alieleza kuwa Ruto alianzisha machafuko alipoona shabaha yake kutwaa madaraka kwa njia ya kura kushindwa.
0 comments: