ROSE NDAUKA: NUSURA WATOTO WANIVUE NGUO
MWIGIZAJI mahiri Bongo, Rose Ndauka amefunguka kuwa amenusurika kuvuliwa nguo na watoto ambao walipandwa na midadi baada ya kumuona ‘live’.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika sherehe ya arobaini ya mwanaye iliyofanyika nyumbani kwao, Tandale-Tanesco, jijini Dar ambapo watoto hao walimvizia Rose alipotoka nje, walimvaa na kuanza kumng’ang’ania nguo.
“Hawakutegemea kuniona pale, wengi wamezoea kuniona kwenye TV. Daah nilipata wakati mgumu kidogo maana ilibaki kidogo wanivue nguo, lakini nashukuru Mungu niliwatuliza, wakanielewa nikarudi zangu ndani,” alisema Rose
0 comments: