WAKILI MAGESA AFARIKI DUNIA GHAFLA WAKATI AKISHUKA KWENYE GARI KWENDA OFISINI..!!
WAKILI wa kujitegemea wa Kampuni ya
Magesa & Company Advocates, Israel Magesa, amefariki ghafla jana
wakati akiteremka kwenye gari alilokuwa akiliendesha.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu
jana, mtoto wake, Phares Magesa, alisema baba yake alianguka ghafla
akiwa anateremka kwenye gari na baada ya kukimbizwa hospitali ilibainika
ameshafariki.
Phares alisema baba yake jana asubuhi
alitoka nyumbani kama ilivyo kawaida kwenda ofisini kwake, akiwa
anaendesha gari yake mwenyewe kabla ya kukutwa na umauti huo saa moja
asubuhi.
“Alikuwa
ameshafika kazini lakini wakati anateremka kwenye gari, alianguka
ghafla, alichukuliwa na kukimbizwa hospitali lakini alipofikishwa
alikuwa tayari amefariki,” alisema Phares.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Ukonga
Majumba Sita, ambako taratibu za mazishi zinaendelea. Mpaka sasa kwa
mujibu wa Phares, familia imekubaliana Magesa aagwe Ijumaa jijini Dar es
Salaam.
Baada ya hapo atasafirishwa kwenda kijiji cha Chitare, Majita, Musoma Vijijini mkoani Mara ambako maziko yatafanyika.
“Tunatarajia
ataagwa nyumbani na kanisani, lakini pia alikuwa ni wakili, hivyo pia
kunaweza kuwa na utaratibu mwingine kutoka kwa mawakili wenzake ambao
watakuwa wameuandaa,” alisema Phares.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: