'SISTER DUU' ALA KICHAPO KIKALI NA KUVULIWA NGUO HADHARANI BAADA YA KUKATIZA MITAANI NA KIMINI HUKO ARUSHA..!!
VIJANA wamechoka kuwaona wanawake wanaovaa kihasarahasara ‘vichupi’
mitaani ambapo wameanzisha oparesheni maalum ya kuwavua kabisa ili
watembee utupu ijulikane moja.
Habari hii inathibitishwa na tukio la
mrembo ‘miss’ (jina lake halikupatikana) ambaye amejikuta katika wakati
mgumu baada ya kukumbana na kasheshe zito kutoka kwa wanaume kufuatia
kinguo kifupi alichokuwa amevaa, kilichoacha nje sehemu kubwa ya mapaja.
JIJINI ARUSHA
Tukio hilo lililovuta umati mkubwa ambalo
lilishuhudiwa na shushushu wetu, lilijiri maeneo ya stendi ya mabasi
madogo jijini Arusha, wiki iliyopita wakati mrembo huyo akiwa na
marafiki zake watatu wakirandaranda kufanya ‘window shopping’.
Mara
baada ya kufika eneo hilo, miss huyo alijikuta akizungukwa na wapiga
debe wa daladala na kuanza kumshushia maneno makali wakimwambia kuwa
wamechoshwa kuona nyeti zao.
AVULIWA
Huku sistaduu huyo akidhani ni kelele za kawaida, wapiga debe hao walimzingira na kuanza kumvua kigauni hicho cheusi.
APEWA KITENGE
Mrembo
huyo alipoona mambo yameharibika huku wenzake wakitoka nduki,
alilazimika kukimbilia katika duka moja la nguo maeneo hayo na kuomba
msaada ambapo alisitiriwa kwa kupewa upande wa kitenge kwa msaada wa
trafiki wa kike aliyemuokoa.
Kabla ya kusaidiwa na trafiki mwingine wa kiume, yule wa kike alimshauri kuvaa kitenge hicho na kuondoka eneo hilo.
AKIMBIZWA
Cha
kushangaza, wakati anatoka katika duka hilo hali ilizidi kuwa tete
baada ya midume walioonekana kuchoshwa na uvaaji wa nguo fupi kumkimbiza
na kuanza kumvua kitenge hicho hivyo kusababisha vurugu kubwa kiasi cha
matrafiki kadhaa kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao.
AJITETEA
Wakati
dada huyo akihojiwa na matrafiki hao, alijitetea kuwa anawashangaa
vijana hao kwa kumfanyia vurugu wakati nguo hiyo siyo fupi na mara
nyingi amekuwa akiivaa na kutembea nayo maeneo kama hayo bila kupata
tatizo lolote.
“Afande hii nguo huwa naivaa sana na sijawahi kupata
matatizo yoyote, sijui leo imekuwaje lakini siyo fupi kama wanavyodai,
nimevaa na kitenge lakini bado wananifanyia vurugu,” alilalamika dada
huyo kwa uchungu.
Licha ya dada huyo kuwa katika mikono ya mmoja wa
matrafiki wa kiume, jamaa hao walizidi kumfuatilia huku wakimrushia
maneno makali ya matusi na wakati mwingine kumsukuma.
Baada ya
trafiki huyo kuona hali inazidi kuwa mbaya, alisimamisha gari moja la
serikali na kumuombea lifti kwa lengo la kumnusuru kufanyiwa kitu mbaya.
TUMEWACHOKA
Wakizungumza
na gazeti hili juu ya tukio hilo, ‘machalii’ hao walisema kuwa
wamechoshwa na uvaaji mbovu wa baadhi ya akina dada ambapo sasa wameamua
kuwafanyia vurugu hizo mpaka hapo watakapoacha kuvaa hovyo.
“Tunakushukuru
kwa kupiga picha, wanatuchosha hawa dada zetu, nguo wanazotuvalia
barabarani ni za kuvaa nyumbani tena chumbani lakini wao wanavaa sehemu
kama hizi, kuanzia sasa kazi itakuwa kama hii hadi watakapoacha, dawa
yao ni kuwawashia moto,” alisema mmoja wa wapiga debe hao huku
akisapotiwa na wenzake.
Siku za nyuma mchezo wa kuwavua nguo fupi
wanawake ulisaidia kupunguza tabia ambapo kwa sasa imerejea kwa kasi
hivyo ili wanusurike na adha hiyo ya kuvuliwa hadharani inayoshika kasi,
inabidi kuvaa kiheshima.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: