AIBU: DAKTARI ANASWA AKIMTOA MIMBA MKE WA MTU NDANI YA JENGO LA CCM..
Daktari Afrika Kweka amenaswa akiwa katika jaribio la kumtoa mimba mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Stella.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye
chumba kilichopo katika jengo la Chama cha Mapinduzi (CCM), Tawi la
Makurumla, Magomeni-Kagera, Dar.
Awali, raia wema wa eneo hilo walituma
malalamiko yao wakidai kwamba, Dokta Kweka amekuwa akifanya ‘mauaji’
hayo ya vichanga waziwazi, hali inayowakera kupita maelezo.
“Jamani hapa Magomeni-Kagera kwenye
jengo la CCM, Tawi la Makurumla, kuna daktari anaitwa Kweka anatoa sana
mimba, hasa wake za watu, njooni mumnase.”
Baada ya kupata taarifa hiyo, uliwekwa
mtego ambapo mmoja wa waandishi wetu wa kike alikwenda kwa Dokta Kweka
na kujifanya mwanafunzi wa chuo lakini ana mimba anataka kuichoropoa.
Mwandishi huyo aliingia na paparazi wa
kiume aliyejifanya ni mpenzi wake aliyempa mimba hiyo. Ndani ya eneo la
tukio walipokelewa kwa bashasha na daktari huyo ambaye alihitaji
shilingi 60,000 kama gharama za kutoa mimba japo baadaye alikubali
kushusha bei hadi shilingi 45,000.
Baadaye daktari huyo alimchukua
mwandishi wetu bila kujua kama hakuwa na mimba wala kitambi na kumpeleka
chumba cha kuchomea sindano ambapo almanusura mpango mzima uharibike
kwa kuwa mwandishi wetu hakupaswa kuruhusu daktari huyo amchome sindano
ambayo ilisadikika kuwa ni ya ganzi.
Hata hivyo, wakati paparazi wetu
akijishauri kuhusu sindano hiyo, ndipo Stella alifika kwenye zahanati
hiyo na kuingia ndani kwa dhumuni la kutoa mimba.
Alipofika aliingia moja kwa moja
chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya ganzi bila woga kisha
akaingia chumba cha kuchoropolea.
Ilikupata uhakika kuwa, mwanamke huyo
ameingia chumba cha kutolea mimba, ndipo ‘wapenzi’ hao (waandishi wetu)
waliwasiliana na wapiga picha wetu waliokuwa chobingo na polisi ambao
walitia timu na kuwanasa.
Daktari huyo na mteja wake walipelekwa
kituo cha polisi na kufunguliwa jalada la kesi namba MMP/RB/567/2013
kosa likiwa kujaribu kutoa mimba huku ikibainika kuwa zahanati hiyo ni
batili kwa kuwa aliisajili kama maabara.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM wa tawi hilo,
Hashim Kimambe alizungumza na gazeti hili juzi na kukiri kuwa taarifa
za kunaswa kwa daktari Kweka anazo.
Alisema: “Hata hivyo, sisi tulikuwa
mbioni kumfukuza kwa sababu alipoomba kupanga hapa alisema anaweka duka
la dawa (famasi), baadaye tukashangaa anaziba watu wanaingia ndani.
“Mbaya zaidi huyu jamaa amekuwa akitumia risiti za CCM katika mambo yake, lazima aondoke kwa kweli, tunamwandikia barua.”
0 comments: