MWIGIZAJI Mkongwe katika tasnia ya filamu bongo Yobnesh Yusuf ‘ Batuli’
ameweka wazi jinsi tasnia ya filamu ilivyo na changamoto nyingi na
kujikuta waliomo humo wanakabiriwa na mitihani mingi hata kwa wale ambao
wangekuwa msaada kwa kuwasaidia na kusonga mbele kisanaa badala yake
uwatolea macho kwa kuwatamani.
“Mimi nasema hata bila uoga kabisa sisi kina dada wa Bongo
movie tuna mitihani kweli kwani hata hao wakubwa wenyewe ambao ndio
msaada ukikutana nao hakuna lolote badala ya kukusaidia kwa kazi yako
anakutongoza na shughuli ndio imeisha, mtu anakuita kwa kigezo cha
kupitia filamu yako lakini mkiona anakutolea macho anakutaka sasa na
wewe filamu hazilipi na unahitaji maisha mazuri,”anasema Batuli.
Msanii huyo anasema kuwa anaona wazi kabisa wasanii wa filamu kufanikiwa
kwa wakati inakuwa ngumu sana kwani kila mtu anataka kuwa kuwatumia kwa
ngono tu kwa sababu anajuwa kuwa wanashida na wanahitaji kutoka, Batuli
anasema kuwa pamoja na kuigiza vizuri lakini fursa bado ni chache kwani
taasisi kama Basata na nyingine hazijui wajibu wake.
Batuli alienda mbali kwa kutolea mifano wasanii kama wa Naijeiria na
nchi zilizoendelea wanavyofaidika na kazi zao bila kutegemea Mapedeshee
hali iliyopo Bongo hata wale ambao wangekuongoza na kukuonyesha njia
wanakutamani na kukutolea macho, pia msanii amedai kuwa tabia hiyo
inashamiri kutokana na baadhi ya wasanii wanapokutana na waheshimiwa
badala ya kuongelea soko la filamu utanguliza shida zao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: