Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

TAULO LA KIPA IVO MAPUNDA LALETA KIZA ZAA SIMBA NA YANGA LEO..LAHUSISWA NA UCHAWI

0 comments


Katika mchezo wa Simba na Yanga Leo Ambao wametoka droo kwa kufungana moja kwa moja palitokea kituko ambacho kimewaacha wengi huo...Kama Kawaida yake Ivo Mapunda akiwa langoni Huwa anakuwa na Taulo kubwa Jeupe la kujifutia Jasho Ambalo hulininginiza Kwenye Nyavu za Goli ..Leo Mchezaji Didie Baada ya Yanga kukosa Goli langoni Hapo aliamua kulichukua Taulo hilo na Kukimbia Nalo na kulitupa kwa Mashabiki ...Kwa kile kinachodaiwa ni Dumba inayozuia Yanga Wasifunge....Ilibidi mchezo usimame kwa muda baada ya kuanza kushikana mashati kuhusu hilo taulo, Mwishowe Taulo lilirudi kwa Ivo Mapunda na Mchezo Kuendelea....

Soma Zaidi»

HAWA NDIO WACHEZAJI WALIOITWA KWENYE TEAM YA TAIFA STAR

0 comments

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho Aprili 20 kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi ambayo itachezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam),Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam) upande wa mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union),Aidan Michael (Ruvu Shooting),Aggrey Morris (Azam),Erasto Nyoni (Azam),Hassan Mwasapili (Mbeya City),Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).
Upande wa Viungo ni Amri Kiemba (Simba),Frank Domayo (Yanga),Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba)na Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji niMohammed Seif Saidi (Kusini Pemba),Ayoub Kasim Lipati (Ilala),Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi),Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 niMbwana Mshindo Musa (Tanga) naBayaga Athanas Fabian (Mbeya).
Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach

Soma Zaidi»

KELVIN YONDANI APOTEA YANGA AKIWA SAFARINI KUELEKEA ARUSHA

0 comments

Beki Kelvin Yondani hajulikani alipo, uongozi haujui na hata benchi la ufundi halitaki kulizungumzia suala Lake. Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa amesema hajui lolote kuhusiana na beki huyo na asingependa kuzungumzia.

“Sina taarifa yoyote kuhusiana na na Yondani,” alisema.

Lakini alipoulizwa bosi wake, Hans ven der Pluijm, naye alisema anachofanya ni kufanya wachezaji waliopo.

“Sasa nisingependa kumzungumzia Yondani, waliopo ndiyo ninafanya nao kazi na nguvu tunaelekeza katika mechi zilizobaki na tunataka kushinda zote,” alisema.

Viongozi wamekuwa wakikwepa kulizungumzia, lakini Yondani inaelezwa aliondoka mara tu baada ya mechi ya Mgambo ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-1 mjini Tanga.

Rafiki wa karibu wa Yondani, amesema kwamba, beki huyo alikasirishwa na kuvishwa lawama alizoona hazikuwa na msingi, kwamba alihujumu kwa kuwa alisababisha penalty iliyozaa bao la pili.

“Unajua yeye ni beki, kosa linaweza kutokea na anaona anaonewa bila sababu za msingi na mbaya kuna baadhi ya viongozi wanaonekana kuungana na wale wasiojua mpira na kusisitiza alisababisha penalty kwa makusudi.

“Sasa hali hiyo imemuudhi na ukizingatia alicheza kwa nguvu sana, alijituma sana siku ile kwa kuwa anajua umuhimu wa ubingwa,” alisema rafiki yake huyo wa karibu bila ya kusema Yondani amejijimbia wapi.

Kabla ya kujiunga na Yanga, wakati huo akiwa Simba, Yondani alikimbilia kwao Mwanza na kujichimbia chanzo likiwa suala la lawama na kushutumiwa kuwa aliifungisha Simba makusudi.

Soma Zaidi»

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YA TANZANIA YACHUKUA KUMBE LA DUNIA

0 comments

Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania jana April 06 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi kwenye mechi hiyo akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0,Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.

Soma Zaidi»

DAVID MOYES AJITETEA ..."HATA INGEKUWA NI FERGUSON MSIMU HUU ANGEPATA WAKATI MGUMU"

0 comments

Meneja wa klabu ya Manchester United, David Moyes amedai kwamba msimu huu wa kwanza kwake hata ungekuwa kwa Sir Alex Ferguson angepata shida kufanya la maana ndani ya msimu ukilinganisha na wachezaji wake wenye umri mkubwa.
“Ukweli nadhai kwamba kama Sir Alex angekua hapa mwaka huu ingekua ngumu kwa Sir Alex pia,nina uhakika hata yeye analijua hilo. Nafikiri watu wanatambua kwamba kuna kikosi ambacho kimepita umri, kwa maana hiyo nadhani ingekua ni msimu mgumu labda kwa yeyote ambaye angekabidhiwa Manchester United mwaka huu,” alisema Moyes

Kauli hiyo ya Moyes imekuja huku Jumamosi hii kundi la mashabiki wa Manchester United likipanga kukodisha ndege itakayopeperusha kibendera chenye maandishi ya kumpinga kocha huyo. Manchester United imekuwa na msimu mbaya kiasi cha mashabiki wa timu hiyo kuanza kulalamika vikali wakimtaka Moyes afutwe kazi.

Soma Zaidi»

KASEJA AMHENYESHA DIDA YANGA

0 comments

UMAHIRI wa kipa, Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’, umemhenyesha Deo Munishi ‘Dida’ ambaye analazimika kukesha mazoezini ili asichuje.

Dida ametamka kuwa ubora wa makipa hao unamfanya afanye kazi ya ziada ambayo anahisi hakuwahi kuifanya katika klabu nyingine zote alizowahi kucheza, pia anaogopa kupigwa benchi na Kaseja kama enzi hizo walipokuwa Simba pamoja.

Kiwango cha Dida kimeimarika kwa sasa na mwenyewe anasema: “Ubora wangu umeongezeka na kuwa juu kwa sababu ya uwepo wa Kaseja na Barthez, ni makipa mahiri kwenye ligi.

“Kwa sababu ya ubora wao, inanifanya nisibweteke, nijitume ili niwe bora zaidi na zaidi. Kama nitabweteka na kuwa chini ya kiwango hata kidogo tu, ni wazi sitapata namba.

“Lakini kama ningekua nacheza kikosi kimoja na makipa wengine wasio na uwezo, lazima ningebweteka kwa sababu ningekosa ushindani na kiwango kingebaki kama kilivyo kwa kukosa changamoto.”

Dida anatarajia kuanza mazoezi mwishoni mwa wiki hii, alikuwa kwenye mapumziko akiuguza kidonda kwenye bega la kushoto.

Alijikata na geti nyumbani kwake, lakini aliibua tatizo lingine baada ya kupakaa dawa ya spiriti nyingi iliyomuunguza na kusababisha kidonda hicho kuongezeka. Yeye amesisitiza anaendelea vizuri na atarudi uwanjani akiwa na kasi hiyo hiyo.

Soma Zaidi»

TAARIFA KUHUSU KUACHISHWA KAZI KWA KOCHA WA TAIFA STARS

0 comments

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.

Soma Zaidi »

MBWANA SAMATTA AMWAGIA SIFA KEDE KEDE MRISHO NGASSA LIGI YA MABINGWA AFRICA

0 comments

Mshambuliaji wa kimataifa mtanzania anayekipiga  TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mtanzania Mbwana Samatta, amesema Mrisho Ngassa wa Yanga amefanya kitu cha maana kwa kupiga ‘Hat-Trick’ mbili mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Samatta alisema idadi hiyo ya mabao si kazi rahisi kwenye mashindano makubwa kama hayo.
Yanga iliifumua Komorozine ya Comoro mabao 12-2 na kuiondosha kwenye mashindano na sasa itaikabili Al Ahly ya Misri ambayo Samatta amesema si timu ya ajabu lakini si laini kama hakuna mipango ya maana.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Lubumbashi, Samatta alisema: “Mabao sita ni mengi sana kufunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ni dalili nzuri kwake na kwa timu.
“Pia yanaashiria mambo mazuri kikubwa, lakini asibweteke kwani anaweza kufanya kitu kikubwa katika mashindano hayo endapo Yanga itafanikiwa kusonga mbele.
“Ngassa ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu, kwangu sioni kitu cha ajabu sana kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja kwa sababu nafahamu uwezo wake, lakini inaashiria pia kwa sasa yuko vizuri sana kimwili na kiakili.”
Kuhusu Yanga na Al Ahly, Samatta alisema: “Al Ahly ni timu kubwa na kama ulivyoona ni mabingwa, lakini mpira ni mchezo wa ajabu, nina imani kama Yanga watajituma, wanaweza kuwavua ubingwa na wao wakasonga mbele.”
Mazembe nayo imo kwenye michuano hiyo na inajiandaa na mechi dhidi ya Astres de Douala ya Cameroon. Kuhusiana na mchezo huo, Samatta ameweka wazi kuwa maandalizi yao ni ya nguvu.
Story kwa hisani ya Mwanaspoti

Soma Zaidi»

KAULI YA MWANASHERIA KUHUSU SAKATA LA OKWI KUICHEZEA YANGA

0 comments

Mwanasheria WA TFF, Allex Mgongolwa amesema kuwa mshambuliaji Emmanuel Okwi yupo huru kucheza Yanga na wala Sakata lake lisipotoshwe. Mgongolwa alisema watu wamekuwa wakipotosha kuhusu Sakata la mchezaji huyo "Hicho kipengele wanachosema kama amecheza klabu mbili kwenye mashindano husika haruhusiwi kucheza klabu ya tatu, kipengele hicho kingepata nguvu kama kungekuwa na zuio la muda, lakni hakuna zuio lolote, ndio maana Fifa wakamruhusu" source Mwananchi

Soma Zaidi»

MCHEZAJI WA YANGA WA ZAMANI ANYONGWA DAR

0 comments

OMAR Changa, straika aliyekuwa na umbo la mwili lililokuwa likiendana na nafasi yake hatunaye, na habari kutoka kwa ndugu zake zinasema alinyongwa na watu wasiojulikana pamoja na kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na ubavuni.

Mchezaji huyo aliyetamba na Yanga alizikwa jana Jumatatu jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar es Salaam huku kifo chake kikiacha maswali mengi ya utata kuliko majibu.

Kwa mujibu wa kaka wa Changa, ambaye alikuwa mchezaji wa Moro United iliyoshuka daraja, kaka wa marehemu Idd Kambi, ameliambiaa Mwanaspoti kuwa kwa mujibu wa ripoti ya daktari aliyokabidhiwa baba wa marehemu, inaonyesha kuwa Omar Changa alichomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni na kilichotokeza mbele ye tumbo huku pia shingo ikionekana kulegea.

“Mpaka sasa tumemaliza mazishi, lakini bado tuna huzuni kuhusu hii ripoti tuliyopewa, tunachofanya tunafuatilia ni timu gani aliichezea mara ya mwisho kwa sababu inaonekana inafichwa, lengo ni kujua mazingira ya mchezo yalikuwaje.”

Mdogo huyo wa marehemu alisema Omar Changa alimpigia simu Jumamosi iliyopita, akimtaka kwenda naye kushuhudia anavyocheza ndondo mchangani maeneo ya Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Changa alifunga bao moja la ushindi kwa penalti.

Mchumba wake marehemu aliyetambulika kwa jina la Sarah Mahemba alisema Changa hakurudi kwake tangu alipoondoka Jumamosi kuelekea Kigamboni katika mchezo huo, jambo ambalo liliwapa shaka wapangaji wenzake siku ya Jumapili na kuamua kumtafuta kupitia simu yake ya mkononi lakini haikupatikana ingawa yeye aliijaribu na kuwa inaita bila kupokelewa mpaka alipopata taarifa za kifo kupitia mdogo wa mshambuliaji wa Mbeya City, Omari Kijuso.

Mwili wa marehemu ulipatikana katika mtaro, maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Soma Zaidi»

HASHEEEM THABEET HALI NI TETE NBA MAREKANI HATARI KUACHIA NGAZI.

0 comments


Mtanzania Hasheem Thabeet amejikuta akikumbwa na hofu ya kupoteza namba yake baada ya mchezaji Steve Adams anayechipukia raia wa New Zealand ambaye amesajiliwa mwaka jana na club ya Oklahoma city thunder alisainiwa na timu hiyo july 2013 mpaka sasa ameonyesha uwezo mzuri hvyo kutishia namba ya Hasheem, tangu asajiliwe amefanikiwa  kufunga point 17 rebounds 10, assist 3 na blocks 3 ambapo ana wastani wa point 3.8 na rebound 4.6... 
Kutokana na umahiri huo kumekuwa na vita ya namba baina ya wachezaji hao

Soma Zaidi»

MAN UTD KAMA KAWAIDA YAO, WALALA 2-1 KWA STOKE CITY

0 comments

Mmmmh Jamani mie sio mshabiki wa Mpira kiivyo ila navyoona na ninavyosikia kila kona Man u jumba limewaangukia mwaka huu kila siku wakicheza lazima wapigwe 2 something ....mmmh wanahitaji maombi tena ya Mwakasege.........Au unaonajeee? tuwakesheeee

Soma Zaidi»

SHAFFIH DAUDA"LEODEGAR TENGA ALI-FAIL BIG TIME KWENYE UTAWALA WAKE TFF-HASA HILI LA MIKATABA MIBOVU"

0 comments


"Nilitegemea Juzi niliposema mikataba mingi iliyosainiwa wakati wa utawala wa Tenga ilikuwa BOMU, cha kusikitisha baadhi ya rafiki zangu humu ndani walikuja na maneno ya kashfa, badala ya kufanya utafiti kwa upande wao kugundua kama nililolisema lina ukweli ndani yake ama la,nadhani sasa baada ya kwenda viwanjani na kujionea hili la Tiketi za electronic mtakuwa mmeanza kuamini maneno yangu niliyoyafanyia utafiti wa kina"

Kauli yake ya Mwanzo:
"Niliwahi kusema Leodegar Tenga kwenye utawala wake wa TFF as an Individual alikuwa mtu poa sana lakini kwenye utawala wake akiwa kama Raisi pale TFF ali-fail big time,alifumbia macho shirikisho kuingia MIKATABA MIBOVU kabisa on Earth." Shaffih Dauda

Soma Zaidi»

MAJANGA:MANCHESTER UNITED YAFUNGWA TENA NA SUNDERLAND KWA MATUTA

0 comments

TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika michuano mbalimbali baada ya kuondolewa na Sunderland katika nusu fainali za michuano ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup iliyopigwa Old Trafford.

Manchester imetupwa nje ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya awali kuwa sare ya 3-3 na Sunderland kushinda kwa penalti 2-1.

Baada ya matokeo hayo, Sunderland inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 18 juu ya Cardiff City katika Ligi Kuu ya England, itakutana na Manchester City Machi 2 mwaka huu katika fainali itakayopigwa uwanja wa Wembley.

Soma Zaidi»

BOND"NILIMPA JACK CLIFF MIL 2 AIGIZE KWENYE MOVIE YANGU AKANISONYA NA KUSEMA HANA SHIDA"

0 comments


MTANGAZAJI wa kituo cha chanel ten Bond Bin Slim ambaeye inadaiwa hivi sasa ni yuko katika mahusiano na mjane wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo marehemu Said Juma Kilowoko “Sajuki”, Wastara Juma amesema siku chache kabla ya mnyange Jack Cliff hajaelekea China ambako alidakwa na dawa za kulevya, alimtolea maneno machafu na dharau na kukataa kupokea kitita cha milioni 2 za kitanzania kama malipo ya kufanya filamu pamoja na Wastara.

Bond alisema kwamba alimpigia simu Jack na kumueleza Ishu hiyo kwani alikuwa miongoni mwa wasanii walioonekana kufaa kucheza filamu lakini mwanadada huyo alimsonya kwa dharau na kumtakia manno machafu na mazito huku akisema hana shida na visenti kama milioni mbili.
“Siongei kwasababu Jack amekamatwa huo ndiyo ukweli.alikataa katakata kupokea pesa hizo na kudai kwamba ni vijihela kwake ambavyo haviangaikii kwa kucheza filamu. Alisema eti mi nimeona hela milioni mbili??” Alifunguka Bond

“Milioni mbili ni pesa nyingi sana kumlipa msanii wa kike hapa Tanzania ili acheze filamu tena vipande vichache. Wasanii wanalilia nafasi hiyo. Nilisikitika sana kwa mtu kama Jack ambaye hana jina kubwa kwenye filamu kukataa tena kwa maneno ya dharau.
“Kukamatwa kwake huko kumenipa picha fulani. Dada zetu wengi wana matatizo sana unapowahitaji kwenye filamu kwasababu wanadai wana pesa nyingi. Hivi kupokea milioni mbili yangu na kubebeshwa mzigo kisha kukamatwa kipi bora??. Alimaliza kwa kusema hayo Bond

Soma Zaidi»

LIGI KUU UINGEREZA::MANCHESTER UNITED WAICHAPA SWASEA GOLI 2 BILA

0 comments
Manchester United halted their three-match losing streak as second-half goals from Antonio Valencia and Danny Welbeck eased the pressure on beleaguered manager David Moyes.
At Old Trafford, where Swansea won for the first time in last weekend's FA Cup tie, the Welsh side were unable to repeat their heroics as United rediscovered the form that earned them six straight wins before that awful start to 2014.

Soma Zaidi»

HIVI NDIVYO WANASOKA WA TANZANIA WANAVYOLIPWA

0 comments


Utafiti wa Mwanaspoti katika klabu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara umeonyesha kuwa klabu tatu; Azam, Yanga na Simba ndizo zinazolipa wachezaji wake mishahara mikubwa zaidi nchini.

Katika wachezaji 13 wanaolipwa zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwezi, Azam imetoa wachezaji watano sawa na Yanga huku Simba ikitamba na wachezaji watatu.

Kundi la kwanza, wanaolipwa mshahara wa milioni 4/= kwa mwezi ni:

Haruna Niyonzim a- YANGA

Kipre Tchetche (Azam), Kipre Balou (Azam), Aggrey Morris (Azam), John Bocco (Azam) Brian Umony (Azam) na Haruna Niyonzima (Yanga).

Kundi la pili, wanaolipwa mshahara wa shilingi milioni 3.6/= kwa mwezi yupo Mbuyu Twite wa (Yanga).

Kundi la tatu la wanaolipwa mshahara wa milioni 3.3/= kwa mwezi wapo Abeil Dhaira na Joseph Owino  (wote wa Simba)

Kundi la nne linalipwa 2.5/= kwa mwezi lina Mrisho Ngassa wa Yanga.

Kundi la tano la wachezaji ambao wanalipwa milioni mbili kwa mwezi ni:
Didier Kavumbagu (Yanga)
Hamisi Kiiza (Yanga)
Amri Kiemba (Simba)
Uchunguzi wa Mwanaspoti, umethibitisha kuwa mshahara wa chini kwa wachezaji wa Azam ni shilingi milioni moja wakati Simba na Yanga ina kundi la wachezaji wanaolipwa kima cha chini cha shilingi laki tatu kwa mwezi.
Mishahara ya wachezaji haikatwi kodi yoyote.

Soma Zaidi»