WEMA: PIGA, UA LAZIMA DIAMOND ANIOE


Na Imelda Mtema
Licha ya mama yake mzazi kupinga kwa nguvu zote, staa wa filamu nchini na mtangazaji wa Kipindi cha Runinga cha In My Shoes, Wema Sepetu ameapa kwamba hata iweje, lazima msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond’ awe mume wake, Amani lina stori kamili.

NI CHAGUO LAKE
Akizungumza na Amani katika spesho intavyu hivi karibuni, Wema ambaye kwa sasa anapika na kupakua na Diamond alifunguka kuwa, amepita kwa wanaume wengi ila anaamini mwanaume huyo ndiye chaguo lake.

Alisema katika uchunguzi wake aligundua kwamba Diamond anampenda kupita maelezo na kwa mapenzi anayomuonesha hana sababu ya kugoma kumpa nafasi ya kuwa mkewe.

“Yaani watu watasema sana lakini piga, ua, garagaza, lazima Diamond anioe. Amekuwa akilizungumzia hilo na kuonesha kuwa yuko ‘siriasi’ hivyo ipo siku historia itaandikwa bila kujali nani atasema nini.

“Unajua mimi ni mtu ninayejitambua na ninayejali maisha yangu hivyo ninapobaini mwanaume f’lani anaonesha kunijali na kunipa mapenzi ninayoyahitaji, kwa nini nisikubali kuingia naye kwenye maisha ya ndoa…?
“Kwa kifupi nampenda Diamond na yeye ananipenda, that’s it,” alisema Wema.

MKWARA WA MAMA YAKE
Kuhusu mama yake kuchimba ‘biti’ kuwa hamtaki Diamond na kamwe hawezi kukubali mwanaye aolewe na mwanaume huyo, Wema alisema:

“Unajua yule ni mzazi, wakati mwingine si mbaya kuonesha hisia zake lakini nitamseti na naamini kwa kuwa ananipenda atakubaliana na mawazo yangu.”

NDOA LINI?
Alipobanwa kuhusu lini watafunga ndoa kwani wamekaa kwenye uhusiano kwa muda mrefu huku wakiachana na kurudiana, Wema alionekana kutokuwa na jibu la moja kwa moja ila akaishia kusema kuwa, siku ikifika kila kitu kitakuwa wazi.

NUKUU YA MAMA WEMA!
Katika sakata hilo, kwa upande wake mama Wema alikuwa na haya ya kusema: “Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani, tena wakiwa na ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond.
“Sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga  mkononi, watakiona cha moto.”
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki, Dar, Diamond aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wema na ikadaiwa kuwa siku nyingi wangeingia katika maisha ya ndoa lakini haukupita muda mrefu wakaachana.

Baada ya kumwagana, Diamond alikwenda kwa mtangazaji wa DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema alihamishia penzi kwa yule kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Clement ‘CK’ kabla ya kumwagana hivi karibuni.
Credits:Global Publishers
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: