MSHINDI WA EBSS ATAYETANGAZWA LEO..KAA TAYARI
Shindano la Epiq Bongo Star Search 2013 linafikia ukingoni leo usiku (November 30), ambapo mmoja kati ya washiriki watano walioingia fainali atatangazwa kuwa mshindi.
Kila mshiriki ana sifa za pekee ambazo zinamtofautisha na washiriki wengine na huenda ikamsaidia kuibuka mshindi.
Jina moja kati ya majina haya litapamba vichwa vya habari kesho. Emmanuel Msuya:
Ni mshiriki namba 21 anaewakilisha kanda ya ziwa. Ndiye mshiriki pekee wa kiume ambaye ameingia fainali akiwa na uwezo mkubwa wa kuimba, lakini kitu kikubwa kinachomtofautisha na wenzake ni uwezo mkubwa alionao wa kupiga vyombo vya muziki kama kinanda na gitaa.
Msuya amerekodi wimbo unaoitwa ‘Leo Leo’ ambao ameufanya na Producer Sheddy Clever. Elizabeth Mwakijambile:
Sifa moja kubwa aliyonayo inayomtofautisha na wenzake ni uwezo wake mkubwa wa kubadili sauti nakuimba vizuri sauti ya base (ya kiume), mbali na vocal ya nguvu ya kike aliyonayo.
Mara kwa mara anapoimba unaweza kuifananisha sauti yake na ya mwanamuziki mkongwe Stara Thomas.
Elizabeth amerekodi wimbo unaoitwa ‘Nifanyeje’ uliotayarishwa na producer Lamar wa Fish Crab. Maina Thadei:
Uwezo mkubwa alionao wa kuimba nyimbo za taarab na miduara umemfanya kuwa na ladha tofauti na wenzake na kujikombea fans wengi wanaopenda aiana hiyo ya muziki.
Sio tu aina ya muziki anaochagua, lakini performance yake awapo jukwaani na mbwembwe za aina yake ni kitu ambacho kitakufanya umuangalie hadi anaposhuka jukwaani.
Maina amefanya wimbo wa mduara unaitwa ‘Panya Buku’, na ukisikiliza utahisi unasikiliza wimbo wa msanii mzoefu kwenye miondoko hiyo.

0 comments: