IGP SAIDI MWEMA ATANGAZA MABADILIKO KATIKA JESHI LA POLISI TANZANIA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wakuu wa Polisi wa Wilaya katika baadhi ya mikoa hapa Nchini.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia usalama wa Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Mayunga ambaye alikuwa Mkuu wa kikosi cha kusimamia mazingira Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha, baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) waliobadilishwa ni pamoja na

aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Tabora ACP Edward Bukombe amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Geita (RCO) ACP Francis Kibona amehamishiwa mkoa wa Njombe kuwa mkuu wa Upelelezi mkoa na nafasi yake inachukuliwa na SSP Simon Pasua kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Wanging’ombe SSP. Francis Maro amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa na aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Katavi ACP. Emmanuel Nley amehamishiwa kikosi cha Polisi wanamaji Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Rukwa SSP. Peter Ngussa amehamishiwa Makao makuu ya Upelelezi Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na SSP Alan Bukumbi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya kati( OCD) Mrakibu wa Polisi (SP) Salum Ndalama anaenda kuwa kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora na aliyekuwa mkuu wa Polisi wa wilaya ya Tunduru (OCD) SP. Amadeus Tesha anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Polisi reli.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na: Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi.

0 comments: