URUSI NA UFARANSA WAZIDI KUMUUMIZA RAIS OBAMA, WADAI SYRIA HAISTAHILI KUVAMIWA NA MAREKANI
Urusi
na Ufaransa zimeeleza wazi wazi tofauti zao kuhusu ripoti ya wataalamu
wa silaha wa Umoja wa Mataifa, ambayo ilithibitisha kwamba silaha za
kemikali zilitumiwa nchini Syria.
Waziri
wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye alikutana na
mwenzake wa Ufaransa Laurent Fabius mjini Moscow jana, alitupilia mbali
madai kwamba serikali ya Syria ndio iliyotumia silaha hizo katika
mashambulizi ya Agosti 21 karibu na Damascus.
Ingawa ripoti hiyo haikusema upande gani ulitumia silaha hizo, Laurent Fabius alisema hakuna shaka lolote kwamba serikali ya rais Bashar al-Assad ndio iliyofanya mashambulizi hayo, ambayo Marekani inasema yaliuwa watu zaidi ya 1400.
Lavrov alisema hakuna ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo, na alikariri msimamo wa nchi yake kwamba silaha hizo zilitumiwa na waasi ili kuzivuta nchi za magharibi ziingilie kati kijeshi.

0 comments: