MWILI WA MAREHEMU MEJA HATIBU SHABAN MSHINDO ALIYEFARIKI NCHINI CONGO WAWASILI ZANZIBAR...
Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefarika Nchini Congo, akiwa katika Jeshi la Kulinda Amani.
Ndege iliobeba Mwili wa Marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo ikiwasili
katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar
ikitokea Dar-es-Salaam.
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijumuika na Ndugu na Jamaa
kuupokea mwili wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo.ulipowasili
Zanzibar kwa mazishi Kijijin kwao Fujoni kwa mazishi jioni hii.
Ofisa wa JWTZ akitowa maelezo ya ratiba ya kuupokea Mwili wa Marehemu
Meja Hatibu Shaban Mshindo katika uwanja wa ndege wa Zanziba leo mchana
na kuzikwa katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Mjane wa Marehemu na Watoto wake wakiwasili katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Abeid Amani Karume leo mchana wakitokea Mjini Dar-es-
Salaam.
WANAJESHI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa na mwili wa Marehemu
Meja Hatibu Shaban Mshindo, baada ya kuuteremsha katika ndege maalum ya
Jeshi.
Wanajeshi wa JWTZ wakitembelea kwa mwendo wa pole wakiwa na Mwili wa
Marehemu Hatibu Shaban Mshindo, baada ya kuwasili Zanzibar, tayari kwa
mazishi yanayofanyika jioni hii katika Kijiji cha Fujoni Wilaya ya
Kaskazini B Unguja.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya ndege vya Zanzibar wakiupokea mwili
wa marehemu Meja Hatibu Shaban Mshindo, aliyefariki Nchini Congo akiwa
katika Jeshi la Kimataifa la kulinda Amani Nchi Congo.
Msafara wa Magari ya JWTZ ukiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume kuelekea katika Msikiti wa Bezredi Muembeladu kwa
kuusalia na maziko yatakayofanyika katika Kijiji chao Fujoni Wilaya ya
Kaskazini B Unguja, saa kumi jioni.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: