MWANAFUNZI AMCHINJA MWALIMU WAKE DARASANI, KISA SIMU YA MKONONI.

Mwanafunzi wa China amemchinja mwalimu wake katika kulipiza kisasi baada ya simu yake ya mkononi kutaifishwa.

Mwanafunzi huyo, aliyetajwa kwa jila la Lei katika taarifa za habari za mjini humo, alibambwa na mwalimu wake, Sun Wakang akiwa anachezea simu wakati wa somo la Kemia katika shule moja mjini Fuzhou, mashariki mwa jimbo la Jiangxi nchini China.


Siku iliyofuata Lei alikwenda kwenye darasa analofundisha Sun ambako mwalimu huyo alikuwa ameketi akisahihisha mitihani, na kumchinja kutokea kwa nyuma.

Mwalimu huyo mwenye miaka 32 ambaye ni baba wa watoto watatu alifariki papo hapo huku mwanafunzi huyo akitokomea kusikojulikana.

Jana Lei alipiga namba ya simu ya dharura na kukiri kuhusika na uhalifu huo kabla ya kujisalimisha mwenyewe polisi mjini Shanghai.

Sun alifanya kazi kama mwalimu wa Kemia katika Shule ya Kati ya Linchuan No. 2 kwa miaka mitano kabla ya mauaji yake ya kutisha, ofisa wa shule Xiong Hainshuo alieleza.

Alikuwa amechukua simu ya mwanafunzi huyo baada ya kijana huyo kuwa akiitumia wakati wa somo, lakini ilirejeshwa mwishoni mwa siku hiyo.

Licha ya hilo, Lei alimshambulia Sun wakati akiandaa masomo ndani ya darasa lake, siku nne tu baada ya Siku ya Walimu wa China, siku ya kitaifa ambapo wanafunzi huwaenzi walimu wao.

Maofisa wanasema mwalimu mwenzake alisikia Sun akilia kwa uchungu na kuita huduma za dharura, lakini mwalimu huyo alikuwa amefariki dunia kabla ya gari la wagonjwa kuwasili.

Nchini China, 'shule ya kati' huchukua miaka 7-9 na 10-12 na ni hatua ya mwisho kabla ya elimu ya juu.

Shule ya Kati ya Linchuan No.2 ni moja ya shule bora katika Jimbo la Jiangxi na ina moja ya wastani wa juu wa kupokea wanafunzi katika eneo hilo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: