RIPOTI YA RAIA MWEMA KUHUSU KUACHIWA KWA MELLISA NA AGNES MASOGANGE..
WATANZANIA
wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward
waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za
dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia
sasa, Raia Mwema limeambiwa.
Ingawa
ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha
kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo
nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika
kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo
katika kundi la dawa za kulevya.
Watanzania
hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver
Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na
thamani ya Sh bilioni 6.8.
Hata
hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha
akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors)
yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za
kulevya.
“Kusema kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo.
"Kama
zingekuwa ni dawa za kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya
waliyokamatwa nayo, sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa
dhamana wakati wowote kutoka sasa,” kilisema chanzo cha kuaminika cha
gazeti hili ndani ya Jeshi la Polisi.
Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika Kusini tangu Julai, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa
zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine,
Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo
katika kundi la dawa za kulevya.
Ni
sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo
zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana
lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.
Vyanzo
vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za
kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa
dhamana.
Kwa
mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya
uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo
zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Gazeti
hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako
lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu
kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
“Unapozungumzia
vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea
unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa
jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya
Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.
“Mtu
anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini
anaweza kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo
kwenye kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali
mbalimbali lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.
“Mtu akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu. Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza.
Hiyo
ndiyo adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya
uhalifu, basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa
maofisa waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya
kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini
China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea
wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za
Kichina.
Mwaka
1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego
Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini
Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya
kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku
michezoni.
Raia
Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika
Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni
Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.
Hata
hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba
Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo
wa molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa
Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.
Akizungumza
na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti
Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao
wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao
kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.
“Haya
mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda
kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo
zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye
thamani ile.
Tunawatafuta
wahusika na tukipata taarifa tutawapa,” alisema Nzowa ambaye anatajwa
kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii dhidi ya dawa ya kulevya.
WATANZANIA
wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward
waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za
dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia
sasa, Raia Mwema limeambiwa.
Ingawa
ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha
kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo
nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika
kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo
katika kundi la dawa za kulevya.
Watanzania
hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver
Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na
thamani ya Sh bilioni 6.8.
Hata
hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha
akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors)
yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za
kulevya.
“Kusema
kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya
kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo. Kama zingekuwa ni dawa za
kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya waliyokamatwa nayo,
sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa dhamana wakati
wowote kutoka sasa,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani
ya Jeshi la Polisi. Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika
Kusini tangu Julai, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa
zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine,
Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo
katika kundi la dawa za kulevya.
Ni
sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo
zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana
lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.
Vyanzo
vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za
kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa
dhamana.
Kwa
mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya
uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo
zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Gazeti
hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako
lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu
kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
“Unapozungumzia
vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea
unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa
jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya
Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.
“Mtu
anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini anaweza
kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo kwenye
kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali mbalimbali
lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.
“Mtu
akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu.
Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza. Hiyo ndiyo
adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya uhalifu,
basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa maofisa
waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya
kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini
China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea
wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za
Kichina.
Mwaka
1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego
Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini
Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya
kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku
michezoni.
Raia
Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika
Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni
Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.
Hata
hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba
Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo wa
molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa
Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.
Akizungumza
na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti
Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao
wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao
kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.
“Haya
mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda
kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo
zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye
thamani ile. Tunawatafuta wahusika na tukipata taarifa tutawapa,”
alisema Nzowa ambaye anatajwa kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii
dhidi ya dawa ya kulevya.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/akina-masogange-kuachiwa#sthash.yvylNO87.dpuf

dhidi ya dawa ya kulevya
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: