KAMBI YA UPINZANI BUNGENI YATISHIA KUTOKUUNGA MKONO MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA KATIBA MPYA....!!
Kambi
ya upinzani bungeni imesema kutokana na mtafuruku uliotokea bungeni kwa
kutolewa nje kiongozi wa kambi hiyo Mh. Freeman Mbowe amesema hawaungi
mkono muswada wa sheria ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2013 kwa
kuwa haiwatendei haki watanzania.
Akizungumza
katika mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Pius Msekwa
bungeni mjini Dodoma kuhusiana na mtafuruku uliotokea bungeni kiongozi
huyo wa kambi ya upinzai bungeni Mh Freeman Mbowe amesema hawatashiriki
katika mjadala huo kwa kile walichodai kuwa chama cha mapinduzi (CCM)
kina ajenda ya siri na kushiriki kwao hawatakuwa wanawatendea haki
watanzania
Akizungumzia
juu ya kile kinachoonekana kwa sasa kuwa ni uhusiano mwema baina ya
chama cha wananchi (CUF) na Chadema,mbunge wa Mkanyageni kupitia CUF Mh
Habib Mnyaa amesema siasa haina adui wala rafiki wa kudumu na hivo
wameungana na Chadema katika kutetea haki,usawa na maslahi ya wananchi
wa Zanzibara na wale wa Tanzania Bara
Katika
tukio jingine wanasheria wa masuala ya haki za binadamu wamesema
kilichotokea bungeni ni kutokana na kitendo cha naibu spika kuchelewa
kutoa majibu ya miongozo kama ilivyoombwa na baadhi ya wabunge na
kuwafanya wabunge wa upinzani kuona wanaburuzwa na kuamua kutoka nje na
kuongeza kuwa hawakufurahishwa na jambo hilo kwa kile alichodai kuwa
mawazo yawachache yanapigwa kumbo
-talkbongo
0 comments: