MASKINI DAZ BABA,ANASWA AKIWA AMEZIMIKA ENEO LA MAKAHABA,UNGA WATAJWA....
MASKINI Daz Baba! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari ya
kusikitisha ya msanii huyo ambaye jina lake kamili ni David Jacob
kunaswa akiwa amezima mjini hapa huku ulevi wa kupindukia ukidaiwa kuwa
chanzo.
Daz Baba au Daz Mwalimu asubuhi ya Agosti 5, mwaka huu alinaswa na
kamera za gazeti hili akiwa hajitambui kwenye eneo maarufu kwa jina la
Itigi lililopo nje ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu ikidaiwa kuwa alifika
mitaa hiyo tangu usiku wa jana yake.
Awali chanzo chetu cha habari kilitupigia simu na kutueleza juu ya
kuzimika kwa msanii huyo aliyekuwa akiunda Kundi la Daz Nundaz Family na
baada ya paparazi wetu kufika eneo la tukio ambalo ni maarufu kwa
biashara haramu ya ukahaba, lilibaini kuwa ni yeye na wasamaria wema
walikuwa wakijaribu kumuamsha bila mafanikio.
“Huyu atakuwa amelewa sana na inawezekana katumia madawa ya kulevya
au kawekewa madawa kwenye bia. Dah! Inasikitisha sana kwa msanii kama
huyu ambaye huko nyuma alikuwa aking’ara kwenye anga la muziki,”
alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa eneo hilo.
Hata hivyo, jitihada za kumuamsha ziligonga ukuta na mpaka paparazi
wetu anaondoka eneo la tukio bado msanii huyo alikuwa hajitambui na
mfukoni hakuwa na kitu, ikiashiria kuwa wahuni walimkomba kila kitu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: