HILI NDIO SAKATA LA IGP MWEMA KUIBIWA UPANGA WA DHAHABU KILO TATU..
Gazeti la Mwananchi limeweka wazi kwamba
upanga wa dhahabu aliokabidhiwa Mwema kama ishara ya kuwa mwenyekiti wa
jeshi kwa kipindi cha mwaka ameshindwa kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya
na iligundulika kuwa uliibiwa siku nyingi na ilibidi akabidhi upanga
feki na kuahidi kwamba ataurudisha baada ya mwezi mmoja ikishindikana
Tanzania itabidi itengeneze upanga mwingine wa dahabu.
Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa
nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga
wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa
nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo
tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni
kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.
Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti
wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali
Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi
wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali
zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa
kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa
hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.
IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo
Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na
kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na
mashirika ya kimataifa.
Upanga huo ambao unakwenda sambamba na
bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi katika nchi husika.
Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO,
vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni
alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa
huo wa kimataifa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa
IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa
kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa
Namibia.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini
kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki
iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili
iliyopita mjini Windhoek.
Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema
alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa
kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni
Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa
uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa
ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au
Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa
kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa
pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na
IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: