"CUF NI CHAMA CHA ZANZIBAR"....TUNDU LISU
Mbunge wa Singida Mashariki mh Tundu Lissu,amesema kuwa CUF ni chama cha
Zanzibar. Akizungumza kipitia Star tv ktk kipindi kiitwacho MEDANI ZA
SIASA NA UCHUMI.
Akihojiwa na mtangazaji wa star tv amesema kuwa hakuna haja ya kutafuta
ushahidi kuhusu hilo kwani tangia kuanzishwa kwa vyama vingi nchini
Tanzania CUF haijawahi kupata wabunge zaidi ya 3 wa kuchaguliwa huku
bara. Hii inaonyesha wazi kwamba CUF ngome yake ni Zanzibar.
Akiulizwa kuhusu CDM kuwa kutokuwa na Wabunge Zanzibar,alijibu kuwa ni
kweli ila ukweli ni kuwa uweze kushinda uchaguzi Tanzania huitaji
kushinda Zanzibar. Kwanza Zanzibar haina hata kura milioni moja zaidi
sana ni kura laki tano,na Jimbo la Ubunge pekee lina zaidi ya kura laki
nne.
Huyo ndie Tundu Lissu Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni. Je yawezekana ni kweli CUF ni chama cha Zanzibar?
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: