AIBU..: DAKTARI FEKI AKAMATWA KATIKA HOSPITALI YA KCMC MOSHI

 

Hali ya wasiwasi imejitokeza kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa huduma za  matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi Kilimanjaro baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumkamata mtu anayejifanya kuwa ni daktari wa watoto akiwa kwenye wodi ya upasuaji.

Daktari huyo feki aitwae Alex Sumni Massawe amewekwa chini ya ulinzi na Jeshi la Polisi baada ya kukutana na mmoja wa wagonjwa ambae alimuahidi kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa ngozi.

 

Alex anadaiwa kutaka kumfanyia upasuaji kijana MAKASI TIPESA mkazi wa Manispaa ya Moshi ambae amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa muda mrefu sasa.

Afisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC Gabriel Chisseo amesema daktari  aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambae amekuwa akijinadi kwamba anafanya huduma hiyo hospitalini hapo.

Chisseo anasema Katika jitihada za wazazi kumuokoa mtoto wao wakawa wamewasiliana na mtu mmoja mtaani aliwapa namba ya huyu daktari feki kwamba angewasaidia, walipokutana nae alisema wamlipe shilingi laki tatu ili afanye huo upasuaji hospitalini KCMC ambapo alitanguliziwa laki mbili za kuanzia


Uongozi wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo aliyekamatwa ndani ya Hospitali hiyo si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake cha kazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha jeshi hilo kumtia mbaroni Alex.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: