Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar
ambaye ni dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na
binti yao wanayemlea.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye
gesti hiyo iliyopo maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00
jioni ambapo Temba ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati
ya Kimara na Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.
Baada ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri
aliitaarifu wanahabari ambapo
alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili
kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
Kwa mujibu wa mke wa Temba, siku
kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa mawasiliano ya kimapenzi kati ya
mumewe na binti yao hivyo akalazimika kufanya uchunguzi wa kina.
Mama Temba alisema kuwa katika harakati zake, siku ya
tukio alifuma ujumbe wa simu ‘SMS’ kwenye simu ya binti huyo, aliposoma
alishtuka kuona ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa mumewe.
Kwa kuwa hakuamini alichokisoma, mama Temba ilibidi amwite binti yake ili amweleze vizuri juu ya ujumbe huo.
Alisema
kuwa binti huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri chini ya miaka 18,
hakuwa na hiyana alimweleza ukweli juu ya tabia ya baba yake huyo
kumtaka kimapenzi.
Aliendelea kusema kuwa alipombana kujua kama ‘walishaduu’, binti huyo alidai kuwa amekuwa akimtolea nje.
Mama huyo alisema kuwa hakuwa na papara mara baada
ya kuambiwa taarifa hizo, alichokifanya alimtaka binti yake huyo
amkubalie na amwambie baba yake huyo wapange wakutane wapi.
Mama huyo alijifanya binti yake na kuanza kuchati na mumewe masuala ya mapenzi bila kufahamu kuwa anachati na mkewe.
Katika
kuchati, Temba alituma SMS: “Tulia natafuta mtu wa kumwachia gari
(daladala) halafu nitakutumia SMS kukuambia tukutane wapi, leo nataka
nifungue ukurasa wa mapenzi na wewe, mwanangu nakuhakikishia utakuwa na
maisha mazuri sana.”
Baada ya kukubaliana kukutana gesti hiyo, mama
huyo alikwenda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo
maeneo hayo ya Kimara-Rombo na kupanga jinsi ya kumnasa.
Majira ya saa 10: 00 jioni, Temba alipata mtu wa
kumwachia daladala na kutinga katika gesti hiyo kisha kumtumia SMS
binti huyo akimtaarifu ameshafika.
Tofauti na alivyotarajia, ujumbe
huo ulitua kwa mkewe ambaye alimwambia binti huyo amfuate mara moja
lakini ahakikishe ‘tunda’ halitafunwi.
Ilidaiwa kuwa binti alipofika
chumbani alimkuta mtu mzima akiwa amevaa taulo tayari kwa kuvunja amri
ya sita na binti yake huyo bila kujua kuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni
kulikuwa na mkewe na polisi.
Ilisemekana waliachiwa kama dakika kumi
na tano ndipo timu nzima ya polisi wakiongozwa na mkewe wakaingia ndani
kwani hawakufunga mlango na ‘shughuli’ ilikuwa bado haijaanza.
Habari
zilisema kuwa mwanaume alipomuona mkewe anaingia chumbani akiwa
ameongozana na polisi nusura apasuke kwa mshtuko kwani alishindwa
kuyaamini macho yake.
Ilielezwa kuwa mume alijaribu kutumia kila aina
ya lugha kumuomba msamaha mkewe lakini mke aliamuru askari kumtaiti kwa
kumpiga pingu na safari ya kwenda kituoni ikaanza.
Kabla ya kupelekwa kituoni jamaa huyo
aliibua timbwili zito na kusababisha watu kukusanyika na kuongoza
msafara kuelekea polisi huku akitembezwa na taulo mtaani huku mkewe
akimbebea nguo nyingine ikiwemo ‘boksa’.
“Yaani hata siamini, mume wangu nilimuamini sana kumbe ananizunguka,” alisema mke wa Temba kwa huzuni.
Alipofika
kituoni, Temba aliandikisha maelezo ambapo hadi mashushushu wetu
wanaondoka eneo hilo, kulikuwa na watu kibao waliokuwa wakipiga kelele.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: