SIMULIZI: MZEE WA MIAKA 80 ATENDEWA UNYAMA WA KUTISHA...... FAMILIA YAKE YATUPWA NJE NA KUBEBEWA VITU VYOTE
MAISHA ya familia ya mzee Athumani Mwenda, 80, ni ya mateso makali baada ya nyumba yao kubomolewa ikiwa na vitu ndani.
Mzee huyo na familia yake sasa wamekuwa wakiishi nje huku wakikabiliwa na njaa pamoja na maradhi mbalimbali.
Tukio la kuvunjiwa nyumba lilitokea Mei 24, mwaka huu katika Kitongoji
cha Mvuti, Ilala, Dar na inadaiwa kuwa ubomoaji huo ulifanyika chini ya
mtu aliyejitambulisha kwa jina la Boatu Msuya ambaye ni dalali wa
mahakama huku akiongozana na polisi sita wenye bunduki aina ya SMG.
Akielezea tukio hilo kwa masikitiko makubwa, mzee Mwenda ambaye ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sangara, Kata ya Msongora alikuwa na
haya ya kusema:
“Sina mahala pa kwenda na hawa watoto, nani anaweza kutupa hifadhi, chakula na matibabu? Tunaishi kama wanyama porini.
“Sijatendewa haki hata kidogo, ni bora wangetuua kuliko kutufanyia
kitendo hiki kilichosababisha tuishi kwa dhiki.
Sidhani kama kuna
mahakama inayotoa amri ya kugawa ardhi yangu bila kutembelea eneo la
tukio, anayedaiwa kuwa ni dalali amegawa na kuchukua eneo kubwa tofauti
na tulivyopatana mahakamani.
“Ni zaidi ya nusu ekari na ndiyo maana
wamechukua na eneo la nyumba yangu na kuibomoa huku nikiwa nimelala
ndani na wajukuu zangu, niliamshwa dakika za mwisho, nikaokolewa na
wajukuu zangu, nusura tufunikwe na kifusi.
“Nilipotoka nje nilikuta
kundi la vijana na askari, niliwauliza kwa nini wananibomolea nyumba,
wakanijibu nikae kimya. Hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekuja
naye wala barua inayonitaka nihame au kubomoa nyumba.
“Ninachokijua ni kwamba tulikubaliana mahakamani kuwa nigawe nusu
ekari ya ardhi yangu ninayoishi nimpe tuliyekuwa naye kwenye kesi
mahakamani.
”Naamini kungekua na watendaji wa mahakama hapa au
kiongozi yeyote wa serikali wa kusimamia zoezi hili haya yote
yasingetokea, nimeonewa.
“Kwa sasa tunalala nje, mvua, jua na
maradhi ni vyetu, nimeishi hapa tangu mwaka 1980 enzi hizo hapa likiwa
pori, leo hii wameona lipo karibu na barabara ya lami wanaamua
kujigawia, sikubali hata kidogo,” alisema.
Afisa Mtendaji wa kata
hiyo, Omar Ali Khalfan alipoulizwa juu ya sakata hilo, alisema kwamba
mzee huyo tayari ameshachukua hatua ya kuandika barua kwenda mahakama
kuu na ameshaipitisha na kumgongea muhuri.
0 comments: