"MUNGU ALINIAMURU NIJIUZULU".. PAPA BENEDICT WA 16.
Rome, Italia. Miezi sita baada ya
kujiuzulu, Papa Benedict XVI, amefungua mdomo na kueleza sababu za
kufikia uamuzi huo wa kushangaza.
Juzi vyombo vya habari vilimkariri Papa Mstaafu Benedict akimweleza mgeni wake kuwa aliitwa na Mungu kwa miujiza.
Kiongozi huyo ambaye alishangaza watu
kwa uamuzi huo wa Februari 8, mwaka huu, hata hivyo alisema sauti ya
Mungu imejibu kupitia kwa mfuasi wake, Papa Francis.
Papa Benedict alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Februari 11, maelezo yake yalielekeza katika afya yake.
Alisema nguvu zake zilikuwa zimepungua kiasi cha kutokuweza kumudu majukumu yake ipasavyo.
Alisema, "Mungu aliniambia 'niondoke,'
nami nikatimiza wajibu huo bila kusita," alisema Papa Benedict ambaye
amekuwa kiongozi wa kwanza kufikia uamuzi huo baada ya miaka 600 ya
Kanisa Katoliki. Alisema tangu wakati huo ameishi maisha ya sala.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 86
alisema ameshuhudia maono ya Mungu kwa miezi kadhaa huku akisikia sauti
na tamaa ya kuendelea kuwa karibu naye (Mungu).
Papa Benedict, hata hivyo alisema
Mungu amembariki na kumwezesha kuuona utukufu wake kupitia kwa Papa
Francis, akielewa kwa nini alitakiwa kuondoka mapema kwa kuitika sauti
na utashi wa Mungu.
Shirika la Habari la Kikatoliki (Zenit), hata hivyo halikueleza ni nani aliyekuwa akizungumza na Papa Benedict.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Papa Benedict imeungwa mkono na vyanzo vya kuaminika kutoka Vatican.
"Ni ripoti ya kuaminika, ina usahihi,
inaeleza mchakato wa kiroho ambao Papa Benedict aliupitia kabla ya
kujiuzulu, vyanzo hivyo vililiambia gazeti la The Times.
Wachunguzi wa mambo wamekuwa wakieleza
kuwa Papa Benedict alikatishwa tamaa na kuvuja kwa siri za mawasiliano
yake binafsi na msaidizi wake
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: