LWAKATARE AKWAMA TENA KUPATA DHAMANA, KESI YA JAYDEE YARUSHWA MPAKA JUNE 13.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare na
mwenziye Ludovick Joseph wamekwama tena leo Jumatatu, Mei 27 kupata
dhamana baada ya Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu, Sundi Fimbo
kueleza kuwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Aloyce Katemana, bado yupo
likizo tangu wiki tatu zilizopita.
Watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka la kupanga njama za kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Lady Jay Dee akiwa na mumewe Gardner Habash wakisuburi kesi kutajwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni leo asubuhi saa tatu.
------------------
------------------
Mwanamuziki Judith Wambura-Habash --Lady Jay Dee-- alifika katika
mahakama ya Kinondoni leo kama ilivyotakiwa kwa mashitaka aliyofunguliwa
hapo. Baadaye amefahamisha kuwa ameambiwa ardui tarehe 13 Juni 2013.
Kesi imetajwa tena tar 13 June 2013. Saa 5 asub.
0 comments: