DIVA WA CLOUDS FM AMPA SUPPORT "MKE MWENZA WA KENYA " ANAYEIWAKILISHA NCHI HIYO KWENYE BIG BROTHER AFRICA
Juzi (May 26) ndio ulifanyika ufunguzi
rasmi wa shindano kubwa Africa la Big Brother ambalo mwaka huu limepewa
jina la “The Chase”, na tayari washiriki wa nchi zote ikiwemo Tanzania
wamekwisha fahamika.
Huddah Monroe a.k.a The boss lady ambaye
ni model mwaka huu ndio amebeba imani za wakenya za kurudi na kitita
cha $300,000 zinazoshindaniwa katika msimu wa 8 wa shindano la Big
Brother “The Chase” baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo ya
jirani.
Siku chache zilizopita jina la Huddah
limeonekana kupata umaarufu zaidi Tanzania hasa kupitia mtandao wa
kijamii wa Twitter, baada ya binti huyo mwenye historia ya matukio mengi
ya utata huko Kenya (pamoja na kujihusisha na upigaji wa picha za
utupu) kujikuta anaingia katika ugomvi wa maneno na mtangazaji maarufu
hapa Tanzania Loveness Love a.k.a Diva kutokana na kinachoaminika kuwa
sababu ni Prezzo.
Diva a.k.a mimi Kupitia akaunti yake ya
twitter, juzi (May 26) aliandika tweet inayoonesha kuweka kando tofauti
alizokuwa nazo na Huddah na kuahidi kumsupport kwa kutokumwandikia
“shit” kama njia ya kumuunga mkono “wifi” katika BBA.
Diva amekuwa akidai kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na rapper kutoka Kenya CMB Prezzo, kitendo kilichopokelewa
tofauti na mrembo Huddah ambaye pia kulikuwa na tetesi aliwahi kudate na
“Liq Her” hit maker, Rapcellency, Prezzo.
0 comments: