Alitaka mimba itolewe sasa anadai mtoto kisa ni wa kiume.
Hii imemtokea binamu yangu, akiwa University alikuwa na boyfriend,
mapenzi ya ujana na ahadi za kuona, ikatokea binamu alipata ujauzito,
akiamini yuko kwenye strong relationship, akamumbia jamaa. Du kusikia
habari hiyo jamaa aliomba mimba itolewe na wamalize shule, waanze kazi
ndio wafanye mipango ya ndoa. Binamu yangu hakutaka kuitoa ile mimba,
tumbo lilivyoanza kuonekana, basi wazazi wake ilibidi wamuulize,
aliwaieleza ilivyokuwa, baba yake ambae ni mjomba wangu alikuwa mkali
sana kwasababu binamu yangu kwa akili za darasani alijaliwa.
Wazazi waliamua kumsaidia mtoto wao, wakampa support yote, alijifungua salama mtoto wa kiume, na wazazi walimchukua mtoto yule akiwa na miezi mitatu, ili binti yao aendelee na masomo. Binamu yangu alimaliza shule na matokeo mazuri sana, alipata kazi, akajiendeleza zaidi na shahada ya uzamili. Hakupata bahati ya kuolewa lakini anamudu kumsomesha mtoto wake katika shule nzuri tu, na maisha yake na mtoto wake ni mazuri sana.
Kijana alitoka kwenye familia nzito, zengwe lilivyotokea, wazazi walimtafutia shule nchi za mbali, akakata mawasiliano na binamu yangu kabisa. Dunia ni duara, amekutana na baba wa mtoto, alimaliza shule na kuoa, yeye na mkewe wamebahatika kupata mabinti wawili, sasa kujua mtoto wa kiume aliye nae ni yule wa binamu yangu tu, anamsumbua sana kutaka mtoto wake, tena kwakuwa binamu yangu hana mume, anajiona anahaki ya kwenda kwake saa yeyote ile. Mpeni ushauri binamu.

0 comments: