NCHI HII INAPOTEZA MWELEKEO WASOMI MKO WAPI?
Ni ukweli usiopingika nchi hii inapoteza uelekeo tofauti na miaka ya 60. Miaka ya 60 hatukuwa na wasomi wengi sana kama maprofesa, madoctor, masters, na bachelors ukilinganisha na ilivyo sasa, chakushangaza nchi ndio inazidi kutumbukia kwenye kila aina ya uovu, na kwa bahati mbaya hakuna hata anayefanya utafiti na kujua tatito ninini.
Miaka ya 60 ilikuwa nafuu kulikuwa na uadilifu tofauti na ilivyo sasa, hivi sasa watoto wanazaliwa wanaanza elimu ya msingi mpaka kufikia vyuo vikuu wakiona wizi, chuki, uongo, fitna.... nikitu cha kawaida tofauti na miaka ya 60. Ukosefu wa uadilifu umefanya ongezeko la wahuni mtaani, mpaka kufikia hatua mtu anashindwa kutofautisha msomi na asiye msomi.
kwa bahati mbaya wahuni hao wanaanza kuingilia polepole sector nyeti ya siasa hapa nchini.
Kila anayelala na kuamka anakwambia namimi nataka kugombea ubunge, matokeo yake tunakuja kupata wahuni wa kisiasa kazi kurushiana matusi majukwani mfano halisi ni mh. Lusinde alipokuwa kwenye kampeni huko Arusha. Pia matokeo yake utakuja kuona wahuni wa kisiasa walivyotaka kuivuruga chadema na kuitana wasaliti huku wakipandikiza chuki kwa wanchi huku sisi tunabaki tunashabikia tukiwapoteza watu muhimu katika ukombozi kwa walio masikini.
Hivi sasa msema kweli ndiye muongo na msema uongo ndiye mkweli.Niseme kwamba chadema ni chama makini sana ila kikihendekeza wahuni wanashinda humu Jf wakipandikiza chuki ndani ya jamii kitapoteza uelekeo.
Umuhimu wa kuwasomesha wanafunzi huku hatuoni faida yao uko wapi? Wengi wanaishia kuwa wanywa pombe, na watu wa vijiweni. Kila aina ya raslimali tunazo wameshindwa hata kutupatia elimu zao tukazalishe, wamesubili ajira wakale rushwa au nao kutamani ubunge wakawe wezi na kupata kiinua mgongo.
By mayange from JF
0 comments: