PINDA AWEKA PINGAMIZI MAHAKAMANI DHIDI YA KESI YAKE.
Kesi hiyo imefunguliwa kwa ushirikiano wa Kituo
cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS).
Katika kesi hiyo, taasisi hizo mbili zinadai kuwa
Pinda alivunja Katiba kwa madai kuwa aliamuru vyombo vya dola kuwapiga
wananchi pale wanapokaidi amri ya polisi na kufanya virugu.
Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji
Kiongozi, Fakihi Jundu, akisaidiana na Jaji Dk Fauz Twaib na Jaji
Augustine Mwarija, limepanga kusikiliza kesi hiyo ilyotajwa kwa mara ya
kwanza jana.
Upande wa walalamikaji uliowakilishwa na mawakili wanne kati ya saba waliotajwa.
Mawakili hao ni, Fulgence Massawe na Harold
Sungusia wanaomwakilisha mdai wa kwanza (LHRC), Rais wa TLS, Francis
Stola, Makamu wa Rais wa TLS, Peter Kibatala, Mpale Mpoki na Jeremiah
Mtobesya wanaomwakilisha mdai wa pili (TLS).
Upande wa wadaiwa Pinda na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, uliwakilishwa na mawakili wakuu watatu wa Serikali. Mawakili
hao ni, Nickson Mtingwa, Sarah Mlipana na Alesia Mbuya.
Hata hivyo upande wa madai uliomba siku 21 kuwasilisha majibu ya majibu ya wadaiwa.
-Mwananchi
-Mwananchi
0 comments: