MTANZANIA ALIYEKAMATWA LOS ANGELES AKIRI KUINGIZA HEROINE MAREKANI
Mtu aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa
miaka 40 jela nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya
dawa aina ya heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).
Shirika la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013
limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa jina la
Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege cha LAX mjini
Los Angeles akitokea Nairobi.
Mackubi alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court)
jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya
Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri kukutwa na dawa hizo
zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya kazi.
Inaripotiwa kuwa maafisa waligundua uzito usio wa kawaida wa
laptop aliyokuwa nayo Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana walipompekua.
Walipompeleka kumpekua kwa mara ya pili kwa kina zaidi, walijaribu kuwasha
komyputa hiyo bila mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina alama za kufunguliwa
awali (tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa ndani ambapo walikuta
gramu 800 za heroin zimefichwa.
Mackubi alisema alikuwa akutane na mwanamke anayeishi jimboni
Alabama, ambaye walifahamiana kwenye mtandao wa internet. Maafisa wamesema kuwa
Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa LAX wakisafirisha dawa za kulevya
kwa njia hiyo.
Hukumu impasayo Mackubi imepangwa kutolewa tarehe 11
Septemba
0 comments: