JOHARI AVAA PETE YA NDOA,IRENE UWOYA AMPONGEZA

MSANII wa filamu za Bongo, Irene Uwoya amempongeza staa mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kutumbukiza picha kwenye Instagram ikimuonesha amevaa pete ya ndoa kwenye kidole husika.

   Uwoya, baada ya kuona picha hiyo akatupia ujumbe wake akisema: Hongera mama kwa kupata mwenzako…maaama h.

Wadau mbalimbali nao walimpongeza Johari kwa hatua hiyo huku wengine wakihoji imekuwaje kimyakimya?

Maswali na pongezi hizo za wadau zilijibiwa na Johari mwenyewe ambaye aliandika:  ‘Thanx ndo maisha yanachange’ (yaani asante ndiyo maisha yanabadilika).
Alipopigiwa simu juzi na kuulizwa kama amefunga ndoa kwa siri, staa huo alicheka na kusema: “Hakuna kitu kama hicho jamani.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments: