MAPENZI YA RAY, CHUCHU HANS NI PIGO!
Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
Ni pigo kubwa! Ile ndoa inayodaiwa kukaribia kufungwa kati ya nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Miss Tanga 2006 aliye pia msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans imepingwa isifungwe mpaka mambo f’lani yakae sawa.
Kwa mujibu wa mtonyaji wetu, Ray na Chuchu wako mbioni kufunga ndoa wakati wowote kuanzi Mei, mwaka huu, lakini mjadala mzito uliopo mbele yao kwa sasa ni uhalali wake.
“Unajua wanachofahamu wao (Ray na Chuchu) wanaweza kufunga ndoa kwa ulaini kabisa, lakini ukweli ni kwamba kuna ugumu mkubwa.
UGUMU ULIPO
“Kanisa analosali Ray, viongozi wanasema wao si wa dunia hii mpaka wakubali kufunga ndoa ambayo mmoja wa wahusika ana ndoa yake,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “Kwa hiyo kama wako tayari kufunga ndoa hiyo lazima Chuchu akubali kubadili dini yeye ndipo ataruhusiwa kungia kanisani kufungishwa ndoa.”
KANISA LA RAY
Juzi Alhamisi, Risasi Jumamosi lilifunga safari hadi kwenye Kanisa la Living Water-Makuti Kawe, Dar ambako mpaka mwaka uliopita magazeti pendwa yaliandika Ray anaabudu huko.
Lengo la Risasi Jumamosi lilikuwa kuonana na Mtume na Nabii Onesmo Ndegi lakini hakuwepo ofisini, ila msaidizi wake mmoja alipopatikana alikiri kumfahamu Ray.
Msaidizi: Ray alishasali hapa, lakini sijamwona siku nyingi, sijui ana matatizo gani?
Risasi Jumamosi: “Oke, tukiacha hilo la kutofika kwa siku nyingi. Lililopo sasa hivi ni kwamba anataka kufunga ndoa na dada mmoja anaitwa Chuchu Hans ambaye ana ndoa tayari, hajaachika na mumewe yu hai. Unasemaje kuhusu hilo?
Msaidizi: “Sisi hatuamini katika kuachana. Kama alishafunga ndoa na mume yupo hai, hao wametengana tu, lakini ndoa yao ipo.
“Huyo mwanamke alishajifunga, kifungo chake kitatenguliwa pale tu mumewe atakapoondoka duniani (kifo).
KANISA LA MTAKATIFU MAXIMILIAN KOLBE
Baada ya kuondoka kanisani hapo, mapaparazi wetu walikwenda Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mwenge, Dar es Salaam.
Risasi Jumamosi liliambiwa Baba Paroko hakuwepo kwa wakati huo, lakini muumini mmoja aliyesema yeye ni mwalimu alipoulizwa kuhusu nafasi ya Ray kufunga ndoa na Chuchu Hans alisema:
“Maandiko yako wazi. Sasa kama huyo mwanamke ana mume wake tena mmesema yupo nje ya nchi, siku akija si atamshika ugoni kwa mke wake?
“Huwezi kufunga ndoa kama bado una ndoa. Mungu hajaagiza hivyo. Ndiyo maana sisi (Wakristo) huwa tunatoa siku ishirini na moja za kutangaza ndoa ili kama kuna mwenye pingamizi ajitokeze na kulianika.
“Watu waongo siku hizi. Wapo wachumba wanakuja kuandikisha ndoa kumbe mmoja bado yupo kwenye ndoa halali.”
IMANI YA KIISLAM INASEMAJE?
Mapaparazi wetu hawakuchoka, walimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum ambaye kuhusu Ray na Chuchu kufunga ndoa alifunguka hivi:
“Kama Chuchu ni Muislam, itabidi Ray abadili dini awe Muislam, si vinginevyo.”
Risasi Jumamosi: Chuchu alifunga ndoa Bomani na mume Mkristo, ila yeye Muislam. Inakuwaje hapo?
Sheke Mkuu: “Itakubalika kama Ray atabadili dini tu, maana hiyo ndiyo ya Bomani, Kiislam siyo.”
JOHARI, MAINDA WAPATANA
‘Johari’ ambaye ni Blandina Chagula na ‘Mainda’ mwenye uhalisia wa jina la Ruth Suka (zamani Mwanaid), wawili hao sasa ni mashosti wakubwa baada ya kuwa na bifu la miaka 8 kisa kikitajwa kuwa ni ‘kaka mkubwa’ huyo (Ray) kuwachanganya kimapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo, mastaa hao wanaotamba kwenye filamu za Bongo kwa miaka mingi wameamua kumaliza tofauti zao huku wengi wakitafsiri kuwa, wanashikamana kwa sababu ya kuumaliza uhusiano wa Chuchu na Ray. Haikufafanuliwa.
MADAI MENGINE
Pia ilidaiwa kuwa, Mainda aliamua kumaliza bifu na Johari kwa sababu mchungaji wake alimtaka kufanya hivyo.
“Niliwakuta kambini wakishuti filamu, Mainda akaniambia aliitwa kushiriki filamu hiyo kama mpambaji, Johari yeye amecheza baadhi ya vipande ndipo Mainda akamtaka mwenzake wamalize tofauti zao,” kisema chanzo chetu.
Hivi karibuni, Risasi Jumamosi liliinasa picha iliyotundikwa mtandaoni na Mainda akimwonesha yeye, Johari na Mtangazaji wa StarTV, Sauda Mwilima.
Mainda aliisindikiza picha hiyo na maneno yaliyosema: “Nimejifunza kitu katika maisha, kusamehe.”
KAKA MKUBWA RAY
Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia simu ya mkononi Ray lakini hakupokea. Akatumiwa meseji, hakujibu!
CHUCHU HANS
Baada ya kusomewa mashitaka yote, alijibu kwa ufupi: “Sina cha kuongea.”
JOHARI
Johari naye hakupokea simu yake ya mkononi licha ya kuita kwa muda mrefu na kukatika kisha kupigwa tena. Akatumiwa meseji, hakujibu!
MAINDA
Na yeye simu yake iliita sana bila kupokelewa, akatumiwa meseji, hakujibu!

0 comments: