"HATUJITOI EAC NG'O"...RAIS KIKWETE
*Ashangazwa na Kagame, Museveni kuitenga Tanzania
*Atofautiana na Membe
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa pamoja na vinavyofanywa na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kuitenga Tanzania, katu haitajiondoa katika jumuiya hiyo.
Pamoja na hali hiyo, Rais Kikwete ameshangazwa na madai kutoka kwa wanachama wa EAC ya kwamba Tanzania haina moyo wala dhamira ya dhati ya kuendeleza utengamano wa Afrika Mashariki.
Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dodoma, alipokuwa akihutubia Bunge ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia hali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
0 comments: