Mbunge
wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya
wabunge, viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu nchini ambao ni
mapapa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Hata
hivyo, Dk. Kigwangallah ambaye amepania kuwataja bungeni watu
wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa
majina hayo kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi
ili kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja.
Miongoni
mwa majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na
wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam.
“Nawashukru wananchi wamenipa ushirikiano hadi jana wamenikabidhi
majina ya watu saba ambao ni wabunge wawili, kiongozi mmoja mwandamizi
wa serikali na wafanyabiashara wanne, ambao wote ni mapapa wauza unga na
siyo madagaa,” alisema Dk. Kingwangallah.
Alisema katika kuhakikisha
anatekeleza alichoahidi amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe
maelezo kwa kuwataja majina vigogo wanaojihusisha na dawa za kulevya na
kwamba bado anasubiri kujibiwa. Dk. Kigwangallah amekabidhiwa majina
hayo siku chache tu baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge),
William Lukuvi, kulieleza Bunge kuwa kama serikali itaamua kutaja
wanaojihusisha na biashara hiyo hakuna atakayesalimika ndani ya bunge
kwa sababu pia wamo wabunge wanaotajwa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments: